Home Kimataifa Mwaka 1 wa ukame wa Messi ugenini katika Champions League

Mwaka 1 wa ukame wa Messi ugenini katika Champions League

4990
0
SHARE

Lionel Messi amefunga jumla ya magoli 16 katika mechi 18 alizocheza msimu huu, lakini anasafiri Jumanne hii kuelekea jijini Turin Italia akiwa na ukame wa mwaka mzima; hajafunga goli katika michuano ya Champions League kwenye mechi zilizochezwa ugenini kwa kipindi cha takribani mwaka sasa.

Messi anahitaji magoli mawili kuweza kutimiza magoli 100 katika mashindano ya ulaya lakini mara ya mwisho kwake kufunga eneo tofauti na Nou Camp katika UCL ilikuwa wakati alipofunga magoli mawili dhidi ya Celtic jijini Glasgow mnamo November 23 mwaka jana.

Tangu hapo, Messi amecheza mechi 4 za ugenini lakini ameshindwa kufunga katika mechi hizo zote. Msimu uliopita, alishindwa kufunga katika mechi za vipigo vya 4-0 vs PSG na 3-0 vs Juventus. Msimu tayari Barca wameshasafiri mara 2, wamecheza dhidi ya Sporting club de Portugal na Olympiakos na mechi zote hizo ukame wa Messi uliendelea.

Katika mechi 4 zilizopita za mashindano yote – La Purga hajaona nyavu hata mara moja. Mara ya mwisho kufunga goli ilikuwa katika dimba la San Mames mnamo Oktoba 28 mwaka huu, lakini ameshindwa kuwafunga Leganes, Sevilla, Olympiakos na Russia ambayo alicheza nayo akiwa na Argentina.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here