Home Kitaifa Muda ambao Nduda anatarajia kuanza mazoezi

Muda ambao Nduda anatarajia kuanza mazoezi

6928
0
SHARE

Taarifa kwamba kocha mkuu wa Simba Joseph Omog ameutaka uongozi wa Simba usajili golikipa katika kipindi hiki cha dirisha dogo zimesambaa kila kona kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari. Sababu kubwa ya Omog kutaka golikipa mwingine inatajwa ni majeraha aliyonayo golikipa Said Mohamed ‘Nduda’ ambapo taarifa hiyo inaeleza golikipa huo ataendelea kuwa nje ya uwanja hadi mwisho wa msimu huu.

Nduda amesema, dakatari aliyekuwa akimuhudumia nchini India alimwambia atanza kufanya mazoezi mepesi baada ya miezi mitatu ambapo anatarajia kuanza mazoezi hayo kuanzia mwezi wa kwanza (January) 2018.

“Daktari wa kule (India) aliniambiwa nitakaa nje kwa miezi mitatu baada ya kufanyiwa matibabu, kuanznia mwezi January mwaka ujao nitaanza mazoezi madogo madogo  lakini sikuambiwa nianze kufanya mazoezi ya kuingia uwanjani”-Said Mohamed ‘Nduda’, golikipa wa Simba.

Golikipa huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar aliumia wakati Simba ikijindaa kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, baadae alisafiri hadi India kwa ajili ya matibabu kisha kurejea nchini. Nduda hajacheza mechi hata moja ya ligi tangu amejiunga na Simba kutokana na kuuguza majeraha kabla hata ya kuanza kwa msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here