Home Kimataifa Listi ya walioshinda mechi zaidi ya 300 La Liga: Iniesta ingizo jipya,...

Listi ya walioshinda mechi zaidi ya 300 La Liga: Iniesta ingizo jipya, Casillas kiboko

3720
0
SHARE

Wakati FC Barcelona ikiendelea kuchanja mbuga kuelekea kuutafuta ubingwa wa La Liga, wakipata pointi 34 katika 36 walizopigania mpaka sasa, Andres Iniesta, mchezaji mkongwe zaidi katika kikodi cha sasa akiwa na miaka 33, bado haonekani kama atachoka mazima hivi karibuni, na jana ameweka rekodi nyingine katika ushindi dhidi ya Leganes – ushindi wa 300 wa La Liga akiwa na Blaugrana.

Ushindi wa kwanza ulianza mnamo December 21. 2002 wakati Barcelona ilipoifunga 4-0, Iniesta akianza na kucheza kwa dakika 59 katika uwanja wa Estadi de Son Moix.

Takribani miaka 15 baadae, Iniesta jana ameshinda mechi ya 300 ya La Liga, na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa 6 kufanya hivyo.

Anayeongoza kwa kushinda mechi nyingi kwenye historia ni Saint Iker Casillas, ameshinda mechi 334, anayefuatia ni Andoni Zubizarreta (333), Raul (327), Xavi (322) na Manolo Sanchis (312).

Kwa maana hiyo gwiji huyu wa Camp Nou ni mchezaji wa 3 wa Barcelona kutimiza idadi hiyo na watano kufanya hivyo akiwa kwenye klabu moja, kwa sababu Zubirazarreta alitumikia Athletic Club na Valencia.

Kiujumla Iniesta ameshinda mechi 71% za La Liga alizocheza, akitoa sare 18% na akipoteza kwa 11%.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here