Home Kimataifa Unaweza kwenda Emirates Stadium kucheki mechi kupitia Arsenal na WorldRemit.

Unaweza kwenda Emirates Stadium kucheki mechi kupitia Arsenal na WorldRemit.

3395
0
SHARE

Club ya Arsenal imeingia mkataba na kampuni inaitwa WorldRemit ikiwa kama mmoja ya wadhamini wake ambao watashirikiana kwenye kazi mbalimbali.WorldRemit ni kampuni ambayo inatoa huduma ya kutuma pesa kidigitali.

Kwa kutumia WorldRemit unaweza kutuma pesa kutoka nchi mbalimbali duniani zikafika moja kwa moja kwenye simu ya mtu unayemtumia. Mfano mtu aliyepo Marekani au nchi za Ulaya, anaweza kukutumia pesa hadi kwenye M Pesa au Tigo Pesa yako.

Arsenal wameingia mkataba wa kufanya kazi pamoja na WorldRemit ili kufikisha huduma hii kwa watu wengi zaidi. Mkuu biashara wa Arsenal Vinai Venkatesham amesema,Ushirikiano huu na WorldRemit chini ya CEO wao ambae ana inspire watu wengi, tuna amini kwa pamoja tunaweza kubadirisha jamii na familia nyingi sehemu mbalimbali duniani. Arsenal na WorldRemit tunavitu vinavyofanana, tunaamini tutafanya kazi pamoja na kupata mafanikio pamoja“.

Moja ya chumba cha ofisi ya WorldRemit

C.E.O wa WorldRemit Ismail Ahmed alisema,Mpira wa miguu ni lugha ambayo kila mtu anaelewa. Nilivyokua nakua ndani ya ardhi ya Somalia, kila siku utaona watoto wanacheza mpira wa miguu hata kipindi cha vita.Ni kitu ambacho kinawaunganisha watu duniani kote, tunajivunia kuwa wadhamini wa club ambayo maono yao yanafanana kwa ukaribu sana na sisi.”

C.E.O wa WorldRemit Ismail Ahmed

Aliendelea, “Ushirikiano huu na Arsenal unaleta fursa kubwa kwetu na tungependa kuwashukuru wateja wetu na hivi sasa tutawaunganisha na watu wengi zaidi duniani. Tunaamini pia kupitia mpira wa miguu tutaongeza fursa mpya pamoja

Huduma ya WorldRemit inaweza kutumia kwa njia ya application ambazo zinapatikana kwenye AppStore na PlayStore.

KUHUSU KWENDA EMIRATES STADIUM

WorldRemit itafanya kampeni ya kuwapeleka mashabiki wa soka kwenda nchini England kuangalia mechi za Arsenal. Nafasi hii itakujia hivi karibuni ambapo kila mshindi atalipiwa kila kitu kuanzia usafiri, hotel hadi kuingia kwenye uwanja wa Emirates kuangalia mechi moja wapo ya Arsenal.

Kuhusu safari hii endelea kufatilia shaffihdauda.co.tz kwa maelezo zaidi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here