Home Kimataifa World Cup 2018: Anguko la Italia, walikosea wapi, hasara za kiuchumi kwa...

World Cup 2018: Anguko la Italia, walikosea wapi, hasara za kiuchumi kwa kuikosa safari ya Russia na Nini kifanyike.

4346
0
SHARE

Wakati Carlo Tavecchio, Rais wa shirikisho la soka la Italia, alipotangaza kupewa kazi kwa Giampiero Ventura kuwa mbadala wa Antonio Conte, alitoa ahadi ya kutengeneza historia ya pamoja.

Mwaka mmoja baadae, kweli wametengeneza historia lakini historia mbaya. Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958, mabingwa wa mara 4 wa dunia hawatocheza kombe la dunia.

Tavecchio mwenyewe amesema kushindwa kufuzu ingekuwa ni janga. Sasa, janga limetokea.

Siku 4 zilizopita zimekuwa siku ngumu kwa Azzurri. Kama kipindi kile Giorgio Chinaglia alipotukana kwenye camera wakati Italia walipotolewa kwenye kombe la dunia 1974, au walipoondoleaa kwenye hatua ya makundi mbele ya New Zealand mwaka 2010 na Costa Rica miaka 4 iliyopita katika michuano ya dunia.

Wapi walipokosea

Kuna taswira mbili ambazo hazitosahaulika haraka machoni mwa wapenzi wa Azzurri. Picha ya Gianluigi Buffon akilia machozi na picha za video zinazomuonesha mmoja wa wasaidizi wa kocha Ventura akibishana Daniele de Rossi – akimuamuru De Rossi kupasha.

“Kwanini niende kupasha?” Alionekana akiuliza De Rossi. “Hatuhitaji sare hapa. Tunahitaji kushinda.” De Rossi akaonekana akimuelekeza kocha wake kwa Lorenzo Insigne – akitoa ishara kwamba ndio anayepaswa kuingia.

Insigne ndio mchezaji fundi aliye kwenye kiwango cha juu kwa sasa katika safu ya ushambuliaji ya Italia. Amekuwa akiiongoza Napoli kuanza msimu wakiwa on fire msimu huu. Lakini Ventura alimuacha nje mshambuliaji wakati timu yake ikimhitaji kuliko wakati mwingine wowote.

Wachezaji wakubwa wa kikosi walikuwa na mkutano wa dharula baada ya sare dhidi ya Macedonia jijini Turin mwezi uliopita. Ripoti zilijitokeza tena wakati timu ilipokuwa ikirejea kutoka kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Sweden ambapo wachezaji wakubwa walimuomba kocha abadili mfumo na uchaguzi wa wachezaji. Inasemekana Ventura alitishia kujiuzulu kabla ya kuombwa kutofanya hivyo.

Mbinu zake zilishindwa kuzaa matunda Jumatatu iliyopita. Wakicheza mfumo wa 3-5-2 ilionekana wazi kwamba hakukuwa na nafasi ya Insigne katika kikosi na ilikuwa wazi baada ya filimbi ya kuanzisha mpira ilipopulizwa kwamba kuwaanzisha mabeki watatu wa kati halikuwa jambo la busara hasa kwa sababu timu pinzani ilikuwa imeweka kambi kwenye eneo lao la penati. Mabadiliko yalihitajika. Italy walikuwa wakipiga krosi kila mara, jambo ambalo halikuwasumbua Wasweden. Mabeki wao warefu walizuia kila krosi iliyopigwa.

Wachezaji ambao wamekuwa na viwango vizuri kwenye timu zao za vilabu, wamekuwa vivuli vyao wakiwa na timu ya taifa, Ventura amekuwa hana mipango na ilianza kujionesha vizuri tangu walipofungwa 3-0 dhidi ya Spain jijini Madrid.

Inatosha kuamini kwamba Italy wametumia mifumo mitatu tofauti katika mechi zao 4 zilizopita. Wachezaji ambao huko nyuma wakipewa nafasi kama Simone Verdi, Jorginho, na Manolo Gabbiadini walipewa nafasi kubwa. Ni Jorginho tu ambaye amekuwa akicheza vyema.

Hasara za kukosa kombe la dunia

Inakadiriwa timu ya taifa ya Azzurri itakosa kiasi cha 100m Euros ambazo zingetokana na mapato ya kufuzu kucheza kombe la dunia. Bonasi kutoka kwa wadhamini, Fedha za mauzo ya haki za matangazo ya Tv na fedha za zawadi. Shirikisho la soka la Italia watapata wakati mgumu wa kujadili mikataba mipya na Luma na wadhamini wao wengine pindi watakapoanza kujadiliana upya.

Haki za matangazo ya TV kwa World Cup zimeshuka thamani kwa zaidi ya nusu ya thamani nchini Italia. Namba ya wateja ya kununua TV – ilipanda kwa 4% wakati wa Euro 2016 – hivi sasa huenda ikashuka.

Mkataba aliovunjiwa Ventura na FIGC unatakiwa pia kulipiwa fidia japokuwa kulikuwa na vipengele vya kuonyesha endapo timu itashindwa kufuzu malipo hayo yatapungua. Ventura aligoma kujiuzulu pamoja na shinikizo kubwa kutoka kwa waitaliano na inaelezwa aligoma kujiuzulu ili asipoteze haki zake za malipo.

Nini kinafuatia

Mara baada ya Ventura kuondolewa, kifuatacho sasa ni kumtafuta mrithi wake. Carlo Ancelotti yupo huru na inaonekana ni muda sahihi kwake kuchukua majukumu ya timu ya taifa.

Wachezaji watatu waliokuwepo wakati Italy iliposhinda taji la kombe la dunia mwaka 2006, Gianluigi Buffon, De Rossi na Andrea Barzagli, wote wameshatangaza kustaafu kuitumikia Azzurri.

Giorgio Chiellini amesema anahitaji muda ili aweze kuamua. Anaamini soka la Italia linahitaji kurudo nyuma kidogo ili liweze kusonga mbele – hapa anamaanisha ku-reset mfumo mzima na kuanza upya.

Haya pia yalisemwa wakati Italia walipotolewa kwenye hatua ya makundi kwenye kombe la dunia lilopita wakati Cesare Prandelli alipojiuzulu, akafuatia Giancarlo Abete. Hata hivyo bado hakukuwa na mabadiliko.

Tavecchio alitoa ahadi ya kufuata mfumo wa Wajerumani na kufungua vituo vya soka nchi nzima. Mpaka anaondoka madarakani vimefunguliwa vituo 30 tu, tofauti na vituo 200 vilivyopangwa mwanzoni.

Ahadi yake nyingine ilikuwa ni kuweka mpango wa kupunguza timu kwenye Serie A kutoka timu 20 mpaka kuwa 18, kuongeza ubora na kuondoa wingi, hili halijaweza kutokea.

Serie A imeanza kuonyesha mwanga wa maisha. Juventus wamefika hatua ya fainali za Champions League mara 2 katika misimu 3. Ukiangalia kwa mfano Premier League, hawajafanikiwa kupeleka timu fainali tangu 2012.

Serie A tayari imeshaipiku Bundesliga katika viwango vya UEFA. Roma waliinyanyasa Chelsea 3-0 katika Champions League, Atalanta waliinyodha Everton katika Europa League 3-0 na Pep Guardiola amesema Napoli ni Moja ya timu bora barani ulaya.

Kuna waitaliano wengi kama Waargentina na Wajerumani katika listi ya wachezaji wanaogombea Ballon d’Or na bado wana kizazi kipya kinachokuja vizuri japokuwa bado hawajafanikiwa kuwapata Totti, Del Piero au Maldini wapya.

Italy walifika nusu fainali ya Euro U21 na katika michuano ya kombe la dunia U20. Kuna mwanga mbele kwenye soka la Italia na kama ambavyo Massimo Gramellini alivyoandika katika Il Corriere della Sera: “Sio mwisho wa dunia, ni mwisho wa kombe la dunia moja”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here