Home Kitaifa Mwantika kucheza mechi ya kwanza VPL 2017/2018

Mwantika kucheza mechi ya kwanza VPL 2017/2018

2833
0
SHARE

Beki wa kati wa Azam David Mwantika hacheza mechi yoyote tangu kuanza kwa msimu huu (2017/2018) ikiwa tayari Aza imeshacheza mechi tisa (9) hadi sasa bila uwepo wake ndani ya uwanja.

Kukosekana kwa Mwantika kwenye kikosi cha kwanza cha Azam kunatokana na ushindani mkubwa wa nafasi katika eneo lake huku wapinzani wake wengi wakiwa ni raia wa kigeni. Kufanya vizuri kwa mabeki raia wa Ghana Yakubu Mohammed na Daniel Amoah ndani ya kikosi cha kocha Aristika Ciaobandiko kunamfanya Mwantika achezee benchi.

Kushindwa kufurukuta kwa Mwantika ndani ya klabu yake, beki huyo wa zamani wa Tanzania Prisons amepoteza nafasi katika timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ambapo mara ya mwisho alicheza wakati Stars ilipocheza ugenini dhidi ya Nigeria (September 2016) kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (Africa Cup of Nations). Baada ya hapo Mwantika aliungana na kikosi cha Azam mkoani Mbeya kwa ajili yamechi za VPL dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City (mechi zote Azam ilishinda uwanja wa Sokoine).

Habari njema ni kwamba, Mwantika huenda akarejea kwenye kikosi cha kwanza kutokana na kukosekana kwa Yakubu. Meneja wa Azam FC Philip Alando amethibitisha Azam itawakosa wachezaji wake watatu wa kikosi cha kwanza (Himid Mao, Yakubu Mohammed na Daniel Amoah) kukosekana kwa Yakubu na Amoah kwa wakati mmoja kutatoa fursa kwa Mwantika kurejea kwenye kikosi cha Azam itakapokuwa ikicheza dhidi ya Njombe Mji siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

Mwantika anatarajiwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza sambamba na  Aggrey  Morris Ambrosi katika beki ya kati, tangu kuanza kwa msimu huu Aggrey amekuwa akicheza na Yakubu, huku walinzi wa pembeni wakiwa ni Daniel Amoah (kulia) na Bruce Kangwa (kushoto).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here