Home Kitaifa Miaka 4 imepita, Simba haijaifunga Prisons uwanja wa Sokoine

Miaka 4 imepita, Simba haijaifunga Prisons uwanja wa Sokoine

6230
0
SHARE

Imepita miaka minne tangu Simba ilipopata ushindi wake wa mwisho dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa nyumbani wa maafande wa jeshi la Magereza, matokeo mazuri kwa Simba katika kipindi hicho yamekuwa ni sare.

Katika mechi tano mfululizo ambazo Simba wamecheza ugenini dhidi ya Tanzania Prisons wameshinda mchezo mmoja pekee, hiyo ilikuwa  20/02/2013 Tanzania Prisons 0-1 Simba. Tangu hapo Simba imekuwa ikitoka kichwa chini kwenye uwanja wa Sokoine kwani tangu kuanza kwa mwaka 2014 hadi sasa bado wanapambana kuupata ushindi wa kwanza tangu waliposhinda kwa mara ya mwisho 2013.

Namba hazidanganyi

Matokeo ya mechi za Tanzania Prisons vs Simba kwenye uwanja wa Sokoine tangu mwaka 2014

 • 09/11/2016 Tanzania Prisons 2-1 Simba
 • 21/10/2015 Tanzania Prisons 1-0 Simba
 • 25/10/2014 Tanzania Prisons 1-1 Simba
 • 09/03/2014 Tanzania Prisons 0-0 Simba

Msimu uliopita Simba ikiwa katika kiwango bora huku ikiuwinda ubingwa, ilijikuta ikichezea kichapo cha 2-1 kama imesimama, licha ya Jamal Myante kutangulia kuifungia Simba bao la kuongoza dakika ya 44 kipindi cha kwanza, Prisons walitoka nyuma na kuzima ndoto za Simba kupata ushindi mbele yao kwenye uwanja wa Sokoine.

Victor Hangaya (kwa sasa yupo Mbeya City) ndio alikuwa mtu mmbaya kwa Simba katika siku hiyo, aliisawazishia timu yake dakika tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili. Wakati Simba wakipambana kuongeza bao la pili ili waondoke na pointi tatu, Hangaya akapachika bao la pili dakika ya lililoimaliza Simba.

Msimu huu Simba wanaingia kuikabili Prisons wakiwa hawajapoteza mechi hata moja tangu kuanza kwa ligi, wameshinda mechi tano na kutoka sare katika michezo minne kati ya tisa, Simba inaongoza ligikwa wastani mzuri wa magoli ikiwa imelingana pointi na Azam (zote zina pointi 19). Prisons yenyewe imeshinda mechi tatu, (imeshinda mchezo mmoja nyumbani katika ya mechi nne) imetoka sare mara tano na kupoteza mchezo mmoja kati ya tisa.

Matokeo ya Prisons kwenye uwanja wa Sokoine msimu huu

 • Tanzania Prisons 2-2 Majimaji
 • Tanzania Prisons 0-0 Ndanda
 • Tanzania Prisons 0-0 Stand United
 • Tanzania Prisons 1-0 Ruvu Shooting

Simba imeshacheza mechi nne nje ya uwanja wa Uhuru kati ya michezo tisa, katika mechi hizo imeshinda mara mbili huku ikitoka sare mbili katika mechi za nje ya uwanja wa Uhuru.

Msimu uliopita Tanzania Prisons ndio ilikuwa timu ya kwanza kuifunga Simba nje ya Dar, kabla ya mchezo huo Simba ilikuwa imepoteza mechi moja (ilipoteza dhidi ya African Lyon uwanja wa Uhuru Dar). Je Prisons itakuwa timu ya kwanza tena kuifunga Simba nje ya Dar?

Matokeo ya Simba nje ya uwanja wa Uhuru msimu huu 

 • Azam 0-0 Simba
 • Mbao 2-2 Simba
 • Stand United 1-2 Simba
 • Mbeya City 0-1 Simba

Utamu wa mechi ya kesho Jumamosi November 18, 2017

Simba watakuwa ugenini kupambana na Tanzania Prisons, mechi hii ina pande mbili, upande wa kwanza Prisons itakuwa ikipambana kuhakikisha inaendeleza rekodi ya kutopoteza dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Sokoine wakati upande wa pili Simba itakuwa ikifanya kila liwezekanalo kuivunja rekodi ya kushindwa kuondoka na pointi tatu mbele ya Prisons kwenye uwanja wa Sokoine.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here