Home Kimataifa Je hii itakuwa Madrid Derby ya mwisho wa Torres?

Je hii itakuwa Madrid Derby ya mwisho wa Torres?

5277
0
SHARE

Endapo Fernando Torres atafanikiwa kucheza katika mchezo wa November 18 katika dimba la Metropolitano – itakuwa Derby yake ya 21 ya Madrid kwa mshambuliaji huyo, swali, Je itakuwa ya mwisho?

El Nino hivi sasa ana miaka 33 na ingawa amepewa mkataba wa nyongeza wa mwaka 1 katika kipindi cha usajili kilichopita, amekuwa akipata nafasi finyu sana ya kucheza chini ya Diego Simeone.

Huku December ikikaribia, Torres amecheza dakika 332 katika mechi 10 zilizopita za mashindano yote na ameanza mchezo mmoja wa ligi, dhidi ya Girona katika mchezo wa ufunguzi wa msimu wa 2017/18.

Katika mechi 3 zilizopita za Atletico katika La Liga, Torres hajacheza hata sekunde na hajafunga goli katika msimu huu. Baada ya kuanza kama mshambuliaji pacha na Griezmann katika mchezo wa Girona, Torres akashuka kwenye listi ya washambuliaji nyuma ya Ángel Correa, Luciano Vietto na Kevin Gameiro.

Torres amekuwa akicheza mchezo wa kusubiri tangu aliporudi Calderon mnamo January 2015. Mara chache amekuwa akipata nafasi ya moja kwa moja akisubiri wengine kuumia ili kupata nafasi.

Mpaka sasa Torres ana historia ya kufunga mara 3 katika Madrid Derby akiwa na uzi wa Atletico. Goli lake la kwanza alifunga msimu wa 2006-07, msimu wake wa mwisho kabla ya kwenda Liverpool. Mengine mawili aliyafunga katika mchezo wake wa kwanza baada ya kurudi akitokea Milan.

Mshambuliaji huyu aliupiga chini mkataba mnono wa kwenda kucheza soka China katika kipindi kilichopita cha usajili na kuamua kubaki Atletico wakati wakihama kutoka Calderon kwenda Metropolitano.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here