Home Kimataifa Griezman anaipenda Atletico lakini Simeone anajaribu kumsukuma kwa Manchester United na Barcelona

Griezman anaipenda Atletico lakini Simeone anajaribu kumsukuma kwa Manchester United na Barcelona

8752
0
SHARE

Katikati ya msimu uliopita jina la mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezman lilitawala sana vyombo vya habari, Griezman alitawala vichwa vingi vya habari akihusishwa na kutimkia Manchester United.

Baadae tetesi zilizimwa huku Antoine Griezman akibaki Atletico Madrid. Lakini miezi michache baada ya dirisha la usajili Griezman anaanza tena kutengeneza habari akitajwa kushindwa kuibeba timu kipindi inachomhitaji.

Atletico Madrid wamekuwa na msimu mbovu sana safari hii huku wakikabiliwa na michezo migumu ndani ya siku saba zijazo ikiwemo mchezo dhidi ya majirani zao Real Madrid na mchezo wa Champions League vs As Roma.

Hadi sasa Atletico Madrid wako nafasi ya katika ligi kuu nchini Hispania La Liga ikiwa ni alama 8 nyuma ya Barcelona na pia kipigo toka kwa As Roma katika mechi ya Champions League kitashuhudia wakiaga michuano hiyo.

Kati ya sababu zilizotajwa kumfanya Antoine Griezman asiondoke Atletico ni kutokana na mapenzi yake juu ya klabu hiyo kiasi cha kuona itakuwa usaliti kuondoka Atletico wakati wanamhitaji sana.

Katika mkataba wa Antoine Griezman na Atletico Madrid kipo kipengele ambacho kimeweka wazi bei ya mchezaji huyo ambapo ilitoka £100m hadi kufikia £200m na sasa itarudi tena £100m mwakani bei ambayo miamba mingi ya Ulaya itatamani kutoa.

Inatajwa kwamba kwa sasa Antoine hana furaha ndani ya Atletico na anatamani kucheza na mwanasoka nguli Lioneil Messi huku pia inatajwa kwamba amekuwa akitamani kujiunga na rafiki yake Paul Pogba katika klabu ya Manchester United.

Griezman amecheza dakika 596 bila goli lakini mashabiki wa klabu ya Atletico wamwkuwa na hamu kubwa kumuona Antoine akibaki tena ili mwakani aanze kucheza na Diego Costa aliyejiunga na Athletico msimu huu akitokea Chelsea.

Diego Simeone amekosa namna ya kumfanya Griezman atakate kwa kukosa kumtaftia pacha sahihi wa kucheza naye kama mshambuliaji hadi sasa huku mechi nyingi ikiwemo ijayo zidi ya Real Madrid akimuacha peke yake kama mshambuliaji wa mwisho mbele.

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps anaona kinachomtokea Griezman kwa sasa (kiwango duni) kinatokana na namna ambavyo timu yake inacheza msimu huu ikiwemo mfumo wa timu na ili kumuokoa ni lazima icheze vyema katika mfumo sahihi.

Kama Atletico watashindwa kucheza vyema kama Dechamps anavyoona baasi hii itamaanisha moja kwa moja itambidi Griezman akatafute mahali ambapo timu itakuwa inacheza vizuri.

Kipigo toka kwa Real Madrid mwishoni mwa wiki kitawafanya kuwa na pengo la alama 11 na vinara wa ligi na kuanza kufuta ndoto zao za ubingwa na kipigo toka kwa As Roma pia kitawafanya kuaga katika makundi ya CL msimu huu.

Wapi atakwenda?Hakuna striker asiyetamani kucheza na Romelu Lukaku kwa sasa na aina ya mshambuliaji kama Griezman aliyejawa na skills ila hayuko vizuri Physically ni lazima atamani kucheza na mshambuliaji mwenye nguvu kama Lukaku na uwepo wa Pogba unawapa nafasi United.

Wakati huo huo kila mchezaji duniani anatamani siku moja acheze pembeni ya kati ya wachezaji hatari kwahi kutokea dunian Ii Lioneil Messi na Griezman naye anatamani hili litokee siku moja.

Real Madrid je? Hapana na siamini kama Griezman atakwenda Madrid kwa kuwa kama ameshaogopa kuwasaliti Atletico kwa timu ya mbali na Hispania ni ngumu akasaini kwa majirani wa Atletico na pia PSG nako tayari kuna utawala mpya itakuwa ngumu kwake kuwa na uhakika wa nafasi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here