Home Kitaifa “Tunasubiri afike ili hatua nyingine zichukuliwe”-Yanga kuhusu Donald Ngoma

“Tunasubiri afike ili hatua nyingine zichukuliwe”-Yanga kuhusu Donald Ngoma

6489
0
SHARE

Uongozi wa Yanga umesema utachukua hatua baada ya mshambuliaji wao Donald Ngoma kurejea nchini akitokea nyumbani kwao Zimbabwe, Ngoma aliondoka nchini kwenda kwao huku uongozi wa klabu hiyo ukiwa hauna taarifa zake za kuondoka.

Dismas Ten ambaye ni afisa habari wa klabu ya Yanga amesema, taarifa za kuondoka kwa Ngoma zinamkanganyiko, uongozi hauna taarifa rasmi za kuondoka kwake hivyo wanasubiri arejee ili wamsikilize kabla ya kuchukua hatua nyingine.

“Ngoma alikuwa Zimbabwe wakati wowote kuanzia sasa anaweza kufika, alikuwa na matatizo ya kifamilia, taarifa za kuondoka kwake ndio zina mkanganyiko. Siku zote mchezaji anapotoka anaaga kwa mwalimu na taarifa zake zinafikishwa kwenye uongozi, hakukuwa na taarifa zake rasmi ofisini, tunasubiri afike ili hatua nyingine ziweze kuchukuliwa.”

“Huwezi kusema jambo tu bila kujua nini kilikuwepo ndani yake, yeye ni binadamu kama wengine kwa hiyo tunapaswa kumsikiliza na kujua nini kilikuwa kina mkabili ili hatua nyingine baada ya hapo ziwezekufuata. Bado ni mchezaji wa Yanga na anatakiwa kuwa kwenye kikosi cha Yanga kwa ajili ya kutimiza majukumu yake.”

Ngoma amecheza mechi nne za kwanza za Yanga msimu huu kati ya tisa, alikosekana kwenye mechi nyingine tano (5) kutokana na kuuguza majeraha aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo alishindwa kuendelea na mchezo huo na kulazimika kupumzishwa. Amefunga magoli mawili katika mechi nne alizocheza msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here