Home Kitaifa Taarifa kutoka Yanga kuhusu Tshishimbi kutakiwa na vilabu vingine

Taarifa kutoka Yanga kuhusu Tshishimbi kutakiwa na vilabu vingine

13553
0
SHARE

Kuna taarifa zinazoeleza kwamba kiungo wa Yanga Pappy Kabamba Tshishimbi anatakiwa na klabu moja ya nchini Afrika Kusini huku pia akitajwa kunyatiwa na klabu ya Azam FC katika kipindi hiki cha dirisha dogo linalofunguliwa leo (Nov 15, 2017).

Taafifa iliyotolewa jana na gazeti moja la michezo nchini imeeleza kuwa, Azam wanataka kutumia upenyo wa Yanga kuyumba kiuchumi ili kumnasa Tshishimbi.

Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema, hadi sasa bado hawajapokea taarifa yoyote mezani kwao kutoka klabu yoyote inayomtaka Tshishimbi.

“Mchezaji kutakiwa na timu ningine si jambo geni, sisi kama klabu hatujapata hiyo taarifa tunasikia kama watu wengine wanavyosikia lakini zitakapofika tutafanyia kazi kwa sababu ni kawaida pia mchezaji kutoka klabu moja kwenda nyingine ni jambo ambalo lipo tangu mpira umeanzishwa duniani kwa hiyo huwezi kumzuia.”

“Hata sisi yupo kwetu kwa sababu alitoka pia timu nyingine kwa hiyo wakati utakapofika tutajua nini kitakwenda kufanyika.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here