Home Kimataifa Kun Aguero apoteza fahamu wakati akiikabili Nigeria

Kun Aguero apoteza fahamu wakati akiikabili Nigeria

4410
0
SHARE

Striker wa Manchester City alipoteza fahamh katika vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mapumziko ya mchezo wa kirafiki kati ya timu yake ya taifa ya Argetina zidi ya timu ya taifa ya Nigeria.

Aguero ambaye alifunga moja kati ya mabao mawili wakati timu yake ikifungea bao 4 kea 3 hapo ja a ilimlazimu kubebea ndani ya gari la wagonjwa kwa ajili ya kwenda hospitali kufanyiwa vipimo zaidi.

Wataalamu wa mambo wamehusisha kuzimia kwa Aguero na ajali ya gari aliyoipata siku chache zilizopita na kusema kwamba huenda mwanasoka huyo bado hajapona vizuri majeraha yake ya mbavu.

Manchester City wenyewe wamekanusha taarifa hiyo wakisisitiza kwamba hakuzimia bali alichoka tu huku shirikisho la soka nchini Argetina hadi sasa likishindwa kutoa taarifa yoyote kuhusu tukio hilo.

Tayari Aguero amepewa ruhusu kurudi nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu zaidi na hakuna uhakika kama atakuwepo mwishoni mwa wiki hii ambapo Manchester City watashuka dimbani kuikabili Leicester City.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here