Home Kitaifa Baada ya watu kusema Tambwe, Ngoma, ‘wanakatwa’ Yanga wamekuja na hii taarifa

Baada ya watu kusema Tambwe, Ngoma, ‘wanakatwa’ Yanga wamekuja na hii taarifa

12315
0
SHARE

Dirisha dogo la usajili linafunguliwa leo Jumatano November 15, 2017 likiwa na dhumuni la vilabu vya madaraja ya chini hadi ligi kuu kufanya maboresho ya vikosi vyao kabla ya mwendelezo wa ligi zinazowakabili, maboresho hayo ni pamoja na kusajili au kuwatema wachezaji ambao hawaisaidii timu au wamekosa nafasi ili kuwapa fursa ya kwenda sehemu nyingine.

Gumzo kubwa kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo limekuwa ni kuhusu mastaa wawili wa Yanga Donald Ngoma pamoja na Amis Tambwe ambao kwa pamoja wanatajwa ‘watakatwa’ katika kipindi hiki. Pia inaelezwa kwamba, kuna uwezekano wa mmoja kutemwa na mwingine kuendelea kukipiga ndani ya klabu hiyo.

“Hakuna sehemu yoyote ambayo Yanga imetoa taarifa hiyo, masuala ya usajili siku zote yanasimamiwa na benchi la ufundi. Mwalimu anapendekeza nani aingie, nani atoke, kwa hiyo atakaporejea tutachukua taarifa yake na kuanza kuifanyia kazi lakini kwa sasa hakuna kauli yoyote kwenye eneo la kuacha au kusajiliwa mchezaji yoyote.”

“Huwezi kuwazuia watu kusema kwa sababu kwenye mitandao ya kijamii ndio sehemu yao kuzungumza na sio jambo geni kwenye mpira wa miguu.”

Taarifa zilizopo ni kwamba, Ngoma yupo kwenye kuti kavu kutokana na kuwa msumbufu kwa tabia zake za kuondoka kwenye klabu bila kuaga hivyo anaweza akawa wa kwanza kupewa mkono wa kwa heri. Kwa upande wa Tambwe yeye majeraha ya muda mrefu ndio yanaweza kumponza kwa sababu hadi sasa bado hajacheza mechi yoyote tangu kuanza kwa ligi msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here