Home Kimataifa Aliyekuwa mume wa Irene Uwoya amefariki

Aliyekuwa mume wa Irene Uwoya amefariki

4354
0
SHARE

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda Hamad Ndikumana akifahamika na mashabiki wa Rwanda kwa jina maarufu la Kataut amefariki usiku wa kuamkia leo.

Ndikumana alikuwa kocha msaidizi wa Rayon Sports ya Rwanda, kocha mkuu wa timu hiyo Olivir Karekezi amethibitisha kifo cha Ndikumana.

“Ni kweli amefariki jana usiku kama saa sita” amesema Karekezi ambaye alikuwa akizungumza kwa shida kutokana na msiba huo.

Ndikumana alikuwa mume wa zamani wa msanii wa Bongo Movies nchini Irene Uwoya na walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume.

Katika kipindi cha uhai wake, Ndikumana alicheza soka la kulipwa kwa muda mrefu nchini Cyprus lakini pia aliwahi kucheza Tanzania katika kikosi cha Stand United mkoani Shinyanga.

Kwa mujibu wa Gwakaya Olivier ambaye ni afisa habari wa Rayon Sports, amesema ugonjwa wa moyo unatajwa kuwa chanzo cha kifo cha Ndikumana.

“Alisikia maumivu makali kifuani akaomba soda ya baridi wakamletea na alipomaliza tu kunywa akatapika na akaishiwa pumzi ndipo akakata kauli”-amesema Olivier lakini akasisitiza bado wanasubiri uchunguzi zaidi wa kitabibu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here