Home Kitaifa Julio ailipua Simba, “wanavuna walichopanda”

Julio ailipua Simba, “wanavuna walichopanda”

11561
0
SHARE

Kocha Jamhuri Kihwelu Julio amesema kwa sasa Simba wanavuna walichokipanda kuhusu usajili wa Shomari Kapombe ambaye tangu amesajiliwa na klabu hiyo bado hajacheza mechi yoyote wala kufanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wengine kutokana na kuuguza majeraha.

Jana Jumatatu Nov 13, 2017 alisikika Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba Zacharia Hans Poppe akisema, Kapombe anatakiwa kuchagua kucheza au kutocheza lakini klabu hiyo haitaendelea kumlipa mshahara huku akiwa hafanyi kazi.

“Simba wanavuna walichopanda, wakati Simba wanacheza ligi wakiwa katika kumalizia mzunguko wa pili wa msimu uliopita, mimi nilipata bahati ya kuwa mmoja ya wachezaji au kocha wa zamani wa Simba nikitunguza na timu kwa ajili yak u-motivate wachezaji na kuwajenga kisaikolojia ili tuweze kufanikiwa nadhani matanda yalionekana kiasi kwamba hata Mavugo ambaye alionekana yupo chini lakini nilijaribu kukaa nae na akaanza kufunga”amesikika Julio kupitia kituo kimoja cha redio.

“Kwa upande wa usajili nilikuwa naulizwa Julio kama kocha nikiwa na wenzangu ambao tulikuwa tunashirikiana lakini kuna watu mpira hawaju ndio wanaivuruga Simba, wanajidai wanamapenzi na timu lakini hawajui mpira ndio wanaiharibu Simba kwenye usajili. Mkikaa kupanga mambo ya wachezaji ukitaja mchezaji ambaye hawamtaki wanahamia ndani lakini watu wote mpira hawajui.”

“Sitaki kuwa mnafiki, kuhusu suala la Kapombe nilikuwepo, wakati wanajadili nilisema hapana labda asajiliwe mwakani lakini alikuja kwa maslahi binafsi. Mimi ndiye nilimfanya Kapombe acheze mpira nimemtoa timu ya Polisi Morogoro akiwa kwenye mashindano ya daraja la kwanza, nilipewa ruhusa hiyo na Msafiri Mgoyi akiwa ni msimamizi wa timu za vijana za taifa wakati huo nilikuwa kocha msaidi wa timu ya U17 chini ya Kim Polsen huku nikiwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya U23.”

“Kwa majeraha aliyokuwa nayo (Kapombe) hakustahili kucheza Simba lakini watu walikuwa wanamtaka kwa sababu ya ubishi wa kutojua mpira, wangekuwa wanatumia waalimu au scouting wanaojua leo wasingefika hapa kwa kutaka kumdhalilisha Kapombe kwa hiyo hili ni zao la mbegu waliyopanda.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here