Home Kimataifa Gianluigi Buffon aangua kilio baada ya kushindwa kuitoa Sweden

Gianluigi Buffon aangua kilio baada ya kushindwa kuitoa Sweden

2771
0
SHARE

Sare ya nunge kwa nunge mjini Milan leo imewafanya wenyeji timu ya taifa ya Italia kushindwa kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia itakayopigwa mwakani.

Sweden wanakata tiketi kulekea michuano hii ya kombe la dunia mwaka 2018 baada ya kupata ushindi wa bao moja kwa nunge katika mchezo uliofanyika siku chache zilizopita.

 Katika mchezo huo ambao Sweden walihitaji alama moja tu ili kufudhu, walifanikiwa kupata alama hiyo baada ya kuzuia nyavu yao isiguswe katika dakika zote za mchezo.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya taifa ya Italia kukosa michuano ya kombe la dunia tangu wafanye hivyo mwaka 1958 wakati michuano hii ilipofanyika Sweden.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here