Home Kimataifa Didier Drogba naye kufuata nyayo za Andrea Pirlo na Xavi Hernandez

Didier Drogba naye kufuata nyayo za Andrea Pirlo na Xavi Hernandez

4455
0
SHARE

Tayari kwa mwaka huu pekee wanasoka wengi manguli wameshuhudiwa wakitundika daluga zao, siku za karibuni Andrea Pirlo, Xabi Alonso na Xavi Hernandez wameamua kuacha kucheza soka na kufanya mambo mengine.

Sasa nguli wa soka barani Afrika ambaye anaichezea timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba naye anaonekana kufuata nyayo za wakongwe hao kwa kuamua kutundika daluga na kurudi nyumbani.

Drogba ambaye kwa sasa anakipiga katika ligi kuu ya nchini Marekani tayari ana umri wa miaka 39 na amekiri kwamba anahisi mwili umechoka na anaona nj bora kukaa pembeni na kuacha maisha mengine yaendelee.

Didier Drogba amekuwa uwanjani kwa miaka 20 sasa na akiwa Chelsea amefanikiwa kutwaa kombe la Epl pamoja na kombe la klabu bingwa barani Ulaya (Uefa) kabla ya mkataba wake kumalizika.

Kwa ujumla Drogba amebeba Epl mara 4, FA cup mara 4, kombe la ligi mara 3, Champions League mara 1, ubingwa wa Uturuki mara 1 huku akifanikiwa kufunga jumla ya mabao 296.

Wakati huo huo Drogba amezungumzia  suala la tajiri wa Chelsea Roman Abromovich kufukuza fukuza makocha ambapo anasema alipomuuliza Roman kuhusu hilo alimjibu kwamba anafukuza ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here