Home Kimataifa Xhaka na Modric nao wakata tiketi ya Urusi 2018

Xhaka na Modric nao wakata tiketi ya Urusi 2018

4176
0
SHARE

Timu zilizofuzu kuelekea kombe la dunia zinazidi kuongezeka baada ya usiku wa leo mataifa mawili ya Crotia na Switzrrland kukata tiketi kwa ajili ya michuano hiyo.

Walianza Switzerland ambao suluhu yao ya bila bila dhidi ya Northern Ireland iliwafanya kufuzu kuelekea kombe la dunia na hii ikiwa mara yao ya 4 mfululizo.

Switzerland wakiongozwa na kiungo wa Arsenal Granit Xhaka wanafuzu katika michuano hiyo kwani mchezo wa kwanza uliopigwa nchini N Ireland waliibuka kidedea kwa bao 1.

Crotia nao baada ya ushindi wa bao 4 kwa 1 vs Ugiriki siku chache zilizopita, leo wamepata suluhu ya bila kufungana iliyowapeleka michuano ya kombe la dunia mwakani

Crotia inakuwa timu ya 28 kufuzu kwa fainali za michuano hiyo na sasa kumebakia timh 4 tu kwa ajili ya kukamilisha idadi kamili ya wanaokwenda kushiriki kombe la dunia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here