Home Kimataifa Sweden watafanikiwa kumstaafisha Buffon bila kombe la dunia machinjoni San Sirro?

Sweden watafanikiwa kumstaafisha Buffon bila kombe la dunia machinjoni San Sirro?

4060
0
SHARE

Italy wapo katika hatari ya kukosa kucheza kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958 ikiwa tu watashindaa kuifunga Sweden katika mchezo wa usiku wa leo utakaopigwa katika dimba la San Siro.

Kikosi cha Giampiero Ventura kilishindwa kupindua matokeo ya 1-0 dhidi ya Sweden pamoja na kucheza vizuri katika kipindi cha pili jijini Stockhlom na leo watakuwa wanahitaji ushindi mkubwa ili kuweza kukata tiketi ya kwenda Russia 2018.

Sweden wao wanajua wakipata goli jijini Milan itawabidi waitaliano wafunge magoli 3 ili waweze kufuzu.

Wasweden waliuanza mchezo wa kwanza kwa kasi katika dimba la Friends Arena, wakishangiliwa na umati wa mashabiki wao. Kikosi cha Janne Andersson kilipata nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza, huku washambuliaji Ola Toivonen na Emil Forsberg walikaribia kufunga mara kadhaa. Dakika

Ya 60 wakapata goli la kuongoza kupitia Jakob Johansson.

Italy walijaribu kusawazisha mara kadhaa, na beki wa Manchester United Matteo Darmian alipiga shuti lilogonga mwamba.

Mchezo wa leo katika dimba la San Sirro unaweza kuwa mchezo wa mwisho wa Gianluigi Buffon kuitumikia Italia katika mechi za mashindano, ikiwa tu Azzuri watashindwa kufuzu. Golikipa wa Juventus ameshathibitisha kwamba ataastafu soka mwishoni mwa msimu, akiombea Italy wafuzu kwenda Russia 2018, na hayo yatakuwa mashindano yake ya 5 ya kombe la dunia kwake.

Mchezaji muhimu wa kikosi cha Ventura – Marco Veratti ataukosa mchezo huu. Kiungo huyo wa Paris Saint Germain amesimamishwa kutokana na kupata kadi ya njano katika mchezo uliopita kwa kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Sweden Marcus Berg. Hivyo kiungo wa Napoli Lorenzo Insigne atachukua nafasi yake.

Kikosi cha Ventura kinahitaji magoli na huenda Simone Zaza akaongoza safu ya ushambuliaji. Mshambuliaji huyo wa Valencia aliukosa mchezo uliopita kutokana na majeruhi ya goti na mpaka sasa hakujakuwa na uhakika wa kucheza kwake.

Upande wa Sweden, Janne Andersson tayari amethibitisha kuwa fiti kwa mchezo na huenda kaanza. Mchezaji wa RB Leipzig Emil Forsberg anatarajiwa kuanza upande wa kulia na anategemewa kuwa mchezaji muhimu zaidi kwa timu yake dhidi ya Azzuri.

Wakati Sweden wakiisaka tiketi ya kwenda Russia 2018 wakiwa wameikosa michuano hiyo tangu 2006, Italy wao hawajawahi kuikosa michuano hii tangu 1958 – zaidi ya miaka 59 iliyopita.

Takwimu za Azzuri katika uwanja wa San Sirro zinaonyesha wamecheza mechi 42 bila kupoteza, wameshinda 31 na sare 11.

Hili linawapa nguvu vijana wa Ventura kuelekea mchezo huu utakaopigwa majira ya saa 4:45.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here