Home Kimataifa Mwandishi aliyeibua Neymar ataondoka Barcelona kaibuka tena, safari hii kasema anakwenda Madrid

Mwandishi aliyeibua Neymar ataondoka Barcelona kaibuka tena, safari hii kasema anakwenda Madrid

9955
0
SHARE

Hali haieleweki kwa mshambuliajiwa Kibrazil Neymar ndani ya PSG, zipo habari zinazodai kwamba Neymar anafurahia maisha yake PSG lakini zipo habari nyingi zinazosema Neymar hana furaha tangu aondoke Barcelona.

Marcelo Bechler alikuwa muandishi wa kwanza kufahamu kwamba Neymar anaondoka Barcelona na ni kati ya waandishi wanaoaminika sana katika masuala ya michezo nchini Brazil.

Bechler ameibuka na mpya ambapo anasema Neymar alipokutana na Luis Suarez na Gerrad Pique aliwaambia kwamba kati ya vitu vinavyomuumiza hivi sasa ni tukio la yeye kuondoka Barcelona.

Bechler amesisitiza kwamba Neymar hapati kile alichotegemea kukipata akiwa PSG kwani uwepo wa wachezaji mastar kama Edison Cavanni, Angel Di Maria unamfanya Neymar akose hashima kama aliyoitarajia.

Lakini pia muandishi huyo ameweka wazi kwamba ni kweli Neynar hana mahusiano mazuri na kocha mkuu wa PSG Unai Emery na hilo pia linamnyima sana Neymar ndani ya timu ya PSG.

Kuhusu tetesi za uhamisho wa Neymar kwenda Real Madrid Bechler amesema ni rahisi sana kwa Neymar kurudi Barcelona kuliko kwenda Real Madrid na kusisitiza kwamba uhamisho wake kwenda Madrid hauwezi tokea kirahisi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here