Home Kitaifa Mayanga ametaja sababu za kumchezesha Himid kama beki

Mayanga ametaja sababu za kumchezesha Himid kama beki

8609
0
SHARE

Yameibuka maswali mengi baada ya kocha wa Stars Salum Mayanga kumchezesha Himid Mao katika nafasi ya ulinzi wa kulia wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin tofauti na ilivyozoeleka kumuona nahodha huyo msaidizi akicheza katika eneo la kiungo wa ulinzi.

Kocha wa Stars Salum Mayanga ametoa sababu za kiufundi zilizopelekea kumpa Himid majukumu ya kucheza kama beki wa kulia wakati kwenye benchi kukiwa na mchezaji Boniface Maganga (Mbao FC) ambaye katika klabu yake anacheza katika nafasi ya ulinzi wa kulia lakini katika mchezo dhidi ya Rwanda kuwania kufuzu michuano ya CHAN uliochezwa CCM Kirumba Mwanza, Maganga aliingia kuchukua nafasi ya Kapombe aliyeumia.

“Baada ya kupata tatizo la Erasto Nyoni nililazimika kuangalia tufanye nini kwenye mechi hii tuliyocheza ugenini, nikaamua ni bora kuongeza viungo wawili lakini nikaweka tahadhali upande wetu wa kulia kwa kumuanzisha Himid kwa kuwa nilikuwa na idadi kubwa ya viungo lakini Himid anaimudu vizuri hiyo nafasi.”

“Kiufundi ni kitu cha kawaida, nimefanya hivyo kwa sababu nilikuwa na uhakika uwezo huo anao na pia kutokana na idadi kubwa ya viungo niliokuwa nao unaweza kuwapangua kulingana na mahitaji ya mechi na timu ikacheza salama.”

“Tumecheza ugenini dhidi ya timu yenye idadi kubwa ya wachezaji wa kimataifa, nililazimika kucheza na watu wenye uzoefu mkubwa ili kuwa salama zaidi katika kuzuia lakini pia katika uwezo wa kumiliki mpira na kushambulia.”

“Kiufundi nilifikia maamuzi hayo kwa faida ya timu na niliyaamini maamuzi yangu ndio maana nikafanya hivyo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here