Home Kimataifa Kikosi bora cha Waafrika waliokosa kombe la dunua

Kikosi bora cha Waafrika waliokosa kombe la dunua

4226
0
SHARE

Tayari nafasi 5 za kwenda kombe la dunia Urusi zimeshapatina huku Nigeria, Tunisia, Senegal, Misri na Morocco wakizichukua, wapo wachezaji hatari kwa sasa ambao wamekwama kwenda kombe la dunia.

1.Dennis Onyango. Onyango amekuwa na kiwango kizuri sana siku za karibuni na ndio maana haikuwa ajabu kwake kupewa tuzo ya mchezaji bora Afrika mapema mwaka huu.

2.Serge Aurier. Alishuhudia nafasi yao ya kufudhu kombe la dunia ikienda kwa Morocco, Aurier amekuwa katika kiwango kizuri kuanzia timu ya taifa  hadi Tottenham Hotspur.

3.Fouzi Ghoulam. Wengi wanamkumbuka katika mechi kati ya Napoli vs Chelsea alionesha kiwango kikubwa sana, lakini pamoja na kiwango bora anachoonesha Napoli ameshindwa kuisaidia Algeria kwenda kombe la dunua.

4.Eric Bailly. Mlinzi wa kati wa Manchester United, Bailly ni kipenzi cha mashabiki wengi wa United lakini naye kama ilivyo Aurier wameshindwa kuisaidia Ivory Coast kwenda kombe la dunia.

5.Joel Matip. Mlinzi kisiki wa Liverpool, hana maelewano mazuri sana na timu yake ya taifa na pia hii inaweza kuwa sababu kwa Matip kutoisaidia Cameroon kwenda kombe la dunia.

6.Jean Seri. Kiungo anayekipiga katika klabu ya OGC Nice ambako tayari vilabu vikubwa vinatajwa kumuwinda ikiwemo Barcelona lakini yeye naye na Ivory Coast watabaki nyumbani kombe la dunia likipigwa.

7.Franck Kassie. Orodha ya mastar kutoka Ivory Coast watakaokosa michuano ya kombe la dunia inazidi kukua, Kassie amekuwa akifanya vizuri nchini Italia tangu alipokuwa Atlanta na sasa Ac Millan

8.Naby Keita. Amekuwa gumzo kubwa katika msimu uliopita wa usajili, bado hakijaeleweka kuhusu uhamisho wake kutoka Rb Leizpg kwenda Liverpool lakimi Keita ameshindwa kuibeba Guinea kwenda kombe la dunia.

9.Yacine Brahime. Kati ya washambualiaji hatari wa Afrika walioko Ulaya ni Brahime, Kwa sasa Brahime anakipiga katika klabu ya Fc Porto lakini ubora wake haukutosha kuibeleka Algeria kombe la dunia.

10.PierreAubemayang. Kwa sasa ndio Muafrika anayecheka na nyavu zaidi barani Ulaya akiwa katika klabu ya Borussia Dortmund lakini hiyo haikusaidia kwake kuipeleka Gabon kombe la dunia.

11.Ryad Mahrez. Winga hatari zaodo katika bara la Afrika, alikiwepo katika kikosi kilichoipa Leicester ubingwa wa Uingereza lakini ameshindwa kuipa Alageria tiketi ya kwenda Urusi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here