Home Kimataifa Heshima kati ya Mourinho na nyota huyu ilianza kuvunjika baada ya Mou...

Heshima kati ya Mourinho na nyota huyu ilianza kuvunjika baada ya Mou kumfananisha na paka

8940
0
SHARE

Jose Mourinho ndio kocha anayeongoza kwa maneno na mara zote amekuwa akisemwa kuwa ni mropokaji, mwaka 2011 katika moja ya mikutano yake na wanahabari Mourinho alitoa kauli ambayo haikumependeza moja ya mchezaji wake.

Alikuwa ni Karim Benzema na katika mkutano huo Jose Mourinho alimfananisha Mourinho na paka, wakati Jose akifanyiwa mahojiano alisema kama nimekosa mbwa baasi nitakwenda kuwinda nikiwa na paka.

Kauli hiyo bado iko kichwani mwa Benzema na hii leo wakati akiongea na jarida moja la michezo alisisitiza kwamba tangu Jose Mourinho atoe kauli hiyo ndipo uhusiano wao ulianza kuvunjika.

Benzema anasema alikuwa akimuheshimu sana Jose Mourinho lakini tangu amfananishe na paka heshima yake kwa kocha huyo ilianza kupungua na hakuwa anamuangalia vizuri toka kipindi hicho hadi sasa.

Karim Benzema amesema yeye ni kijana mpole sana lakini kama utamfanyia kitu hakipendi hawezi kuwa mpole tena ila kama utamuheshimu baasi heshima itakuwepo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here