Home Kitaifa Afya ya Kapombe yazua ‘kizaazaa’ Simba

Afya ya Kapombe yazua ‘kizaazaa’ Simba

5394
0
SHARE

Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba Zacharia Hans Poppe ameibuka na kusema beki wao wa kulia Shomari Kapombe anatakiwa kuchagua kucheza au kutocheza lakini wao hawawezi kuendelea kumlipa mshahara wakati hafanyi kazi anayotakiwa kuifanya.

Poppe amekiri kwamba, walimsajili Kapombe kwa sababu walikuwa wanamhutaji lakini kama bado hajapona majeruhi yake inabidi wakae na kuzungumza kuona wanafanyaje kuhusu hilo.

Kuhusu tetesi za beki kutemwa katika kirisha dogo la usajili, Poppe amesema, hiyo itakuwa ni juu yake mwenyewe (Kapombe) kama amepona acheze kama hawezi basi.

“Hiyo itakuwa juu yake mwenyewe, kama amepona acheze kama hawezi basi, huwezi kumlipa mtu mshahara wakati hafanyi kazi inayotakiwa kufanywa.”

“Inategemea nay eye mwenyewe, kama anataka kucheza acheze, hataki ahame sio anakula hela bure. Majeruhi gani yasiyopona muda wote huo? Kama majeruhi basi akae pembeni hadi apone kwa sababu hii ni kazi ambayo mtu unahitaji kutumia mwili wako kama mwili hauwezi sasa utamlipa mshahara wa kazi gazi.”

“Vipimo vinaonesha amepona vizuri tu, lakini yeye anaweza kuwa anaogopa ataumia, sasa ni yeye mwenye aamue anacheza au hachezi.”

Kapombe alisajiliwa na Simba kabla ya kuanza kwa msimu huu baada ya kumaliza mkataba wake na Azam lakini ameshindwa kucheza mechi yoyote kutokana na kuuguza majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa kwanza kuwania kucheza michuano ya CHAN dhidi ya Rwanda uliochezwa July 15, 2017 uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

July 18, 2017 www.shaffihdauda.co.tz ilizungumza na daktari mkuu wa Taifa Stars Richard Yomba ambaye alisema, Kapombe alihitaji uchunguzi kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili na hakuwa miongoni mwa wachezaji waliosafiri kwenda Rwanda kwa ajili ya mchezo wa marudiano July 23, 2017.

“Kapombe yupo kwenye matibabu ya awali ya saa 72, kutokana na hali yake ya sasa hatoweza kushiriki mazoezi na wenzake. Tukifika Dar tutamkabidhi kwa mwenyekiti wetu wa tiba ili aweze kupata uchunguzi zaidi MOI Muhimbili” – Richard Yomba, daktari wa timu ya taifa ‘Taifa Stars. (July 18, 2017)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here