Home Kimataifa Mrembo ajitokeza na kusema alitembea na Cr7 wakati mpenzi wake ni mjamzito

Mrembo ajitokeza na kusema alitembea na Cr7 wakati mpenzi wake ni mjamzito

7515
0
SHARE

Cristiano Ronaldo anasifika kwa kiwango chake uwanjani na ufungaji wake wa mabao lakini nje ya uwanja pia Mreno huyo ana sifa nyingine kubwa ambayo ni kutembea na warembo kila kukicha.

Wakati dunia ikisubiria mtoto wa Cr7 wa nne ambaye aatakuwa mtoto wake wa kwanza kuzaliwa na mama anayefahamika(Georgina Rodriguez), kumeibuka mrembo mwingine na kudai alilala na Cristiano Ronaldo.

Natacha ni mrembo ambaye ni mtangazaji wa runinga amejitokeza na kuongea na jarida moja la michezo kwamba Ronaldo alitembea naye na baada ya muda aliamua kumblock na kumpotezea.

Natacha amedai kwamba yeye na Cr7 walikuwa marafiki sana na muda mwingi waliutumia kuwasiliana na ndipo usiku mmoja walilala pamoja kisha binti huyo alimuambia Ronaldo mpango wake kwenda nchini Ureno.

Binti huyo anasema Cristiano hakupenda yeye aende Ureno na siku hiyo hiyo baada ya kulala naye ndipo Ronaldo akamblock na sasa Natacha anaamini kwamba Ronaldo alimuhitaji tu ili kumtumia.

Pamoja na kupotezewa na Cristiano Ronaldo lakini mlimbwende huyo amesisitiza kwamba hajutii kitendo alichofanyiwa na mwansoka huyo bora wa dunia bali anaona ndoto zake zimekuwa kweli.

Ronaldo alionekana kutulia sana kimapenzi tangu aanze uhusiano na Georgina lakini habari hizi huenda zikaanza kuchafua hali ya hewa katika uhusiano wa wapenzi hao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here