Home Kitaifa Mechi 13 za Taifa Stars chini ya Salum Mayanga tangu March 2017

Mechi 13 za Taifa Stars chini ya Salum Mayanga tangu March 2017

5828
0
SHARE

Leo November 12, 2017 kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinacheza ugenini dhidi ya Benin mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA, ni mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa Stars chini ya Salum Mayanga kucheza nje ya Tanzania. Kabla ya hapo mechi zote za kirafiki zilikuwa zikichezwa uwanja wa nyumbani.

Stars inaingia kwenye mchezo huo chini ya Mayanga ikiwa imecheza mechi 13, imeshinda michezo 6, sare 6 huku ikiwa imepoteza mchezo mmoja tu. Katika mechi hizo Stars imefunga jumla ya magoli 15 na kuruhusu kufunga magoli 9 na kufanya wastani wa magoli kuwa 6.

Mechi 13 ambazo kocha Salum Mayanga ameiongoza Stars tangu alipokabidhiwa juku hilo kutoka kwa Charles Boniface Mkwasa

 • Tanzania 2-0 Botswana (mechi ya kirafiki ya kimataifa)
 • Tanzania 2-1 Burundi (mechi ya kirafiki ya kimataifa)
 • Tanzania 1-1 Lesotho (kufuzu AFCON)
 • Tanzania 2-0 Malawi (COSAFA)
 • Angola 0-0 Tanzania (COSAFA)
 • Tanzania 1-1 Mauritius (COSAFA)
 • Afrika Kusini 0-1 Tanzania (COSAFA)
 • Zambia 4-2 Tanzania (COSAFA)
 • Tanzania 0-0 Lesotho (Stars ilishinda kwa penati 4-2 COSAFA)
 • Tanzania 1-1 Rwanda (kufuzu CHAN)
 • Rwanda 0-0 Tanzania (kufuzu CHAN)
 • Tanzania 2-0 Botswana (mechi ya kirafiki ya kimataifa)
 • Tanzania 1-1 Malawi

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here