Home Kitaifa Maguri kakabidhiwa majukumu ya Samatta

Maguri kakabidhiwa majukumu ya Samatta

3267
0
SHARE

Baada ya mshabuliaji Mbwana Samatta kukosekana kwenye kikosi Stars kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi Benin, kocha mkuu wa timu hiyo Salum Mayanga amesema majukumu yote ya Samatta yatabebwa na mshambuliaji Elias Maguri.

“Kutokuwepo kwa captain (Samatta) kutokana na tatizo alilolipata la maumivu, nafasi yake atacheza Elias Maguri na baadhi ya maeneo ya Erasto Nyoni na Mzamiru Yassin tumeweza kuangalia kwa macho mawili nafasi zao na tumeziziba”.

“Kwa kifupi tutacheza vizuri mcherzo wetu dhidi ya Benin na matumaini ya kufanya vizuri yapo kwa sababu vijana wetu wapo kwenye ari na kuona tunaendelea kucheza vizuri na timu yetu kuimarika kiufundi.”

Wachezaji ambao hawapo kwenye kikosi cha Stars utokana na sababu mbalimbali ni Mbwana Samatta na Farid Mussa (wanauguza majeraha) Mzamiru Yassin na Erasto Nyoni (wanatumikia adhabu ya kadi nyekundu.)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here