Home Kitaifa Simba, Yanga, kurejea taifa

Simba, Yanga, kurejea taifa

4137
0
SHARE

Leo November 11, 2017 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiambatana na kamati ya maandalizi ya fainali za Afrika (AFCON U17) amefanya ziara ya kutembelea uwanja wa taifa kukagua ukarabati unaoendelea katika eneo la kuchezea (pitch) na maeneo mengine.

Dkt. Mwakyembe ameishukuru kampuni ya SportPesa ambayo ndio imebeba jukumu la kukarabati uwanja huo.

“Nashukuru kuona nyasi za uwanjani zimeota vizuri na unapendeza, kikubwa nashukuru kwa vijana wetu sita ambao wamefundishwa namna ya kutunza viwanja”-Dkt. Mwakyembe.

Mkuu wa oparesheni SportPesa Luca Neghesti amethibitisha ukarabati wa uwanja utakamilika November 21 na utakabidhiwa November 24 mwaka huu ukiwa tayari kwa matumizi.

“Kazi ya kukarabati sehemu ya kuchezea imekamilika na nyasi zilizooteshwa zimeota vizuri na zimeshika hivyo upo tayari kutumika,” alisema Luca.

Vilabu vya Simba na Yanga ambavyo huutumia uwanja wa taifa kwa mechi zao za nyumbani huenda zikarejea kwenye uwanja huo kuanzia November 24 baada ya kukabidhiwa kwa serikali. Vilabu hivyo vililazimika kutumia uwanja wa Uhuru kwa mechi zao za nyumbani kupisha matengenezo yanayoendelea uwanja wa Taifa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here