Home Kimataifa Miamba miwili ya kiarabu yakamilisha idadi ya wawakilishi wa Afrika kuelekea Urusi...

Miamba miwili ya kiarabu yakamilisha idadi ya wawakilishi wa Afrika kuelekea Urusi mwakani

7055
0
SHARE

Miamba miwili toka Afrika timu ya taifa ya Morocco na Tunisia imekata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi mwakani baada ya kupata alama katika michezo yao ya leo.

Tunisia walihitaji alama moja tu ili kwenda kushiriki michuano hiyo na wamefanikiwa kupata alama moja baada ya hii leo kulazimisha suluhu ya bila kufungana dhidi ya timu ya taifa ya Libya.

Suluhu ya leo ya Tunisia imewafanya kufikisha idadi ya alama 14, alama ambazo Dr Congo wameshindwa kuzifikia huku leo wakilazimishwa suluhu ya bao moja kwa moja dhidi ya timu ya taifa ya Guinea.

Morocco kwa upande wao wamekata tiketi kuelekea kombe la dunia baada ya kuwafunga Ivory Coast kwa jumla ya mabao 2 kwa nunge katika mchezo uliokua wakuamua nani wakwenda kombe la dunia kutoka Grouop C.

Alianza Nabir Dirar dakika ya 25 kuwapa wageni bao la kuongoza, wakati Ivory Coast wakijipanga kusawazisha dakika 5 baadae Medhi Benatia aliwapa wageni bao la pili lililowahakikishia tiketi kuelekea Urusi.

Kwa matokeo hayo sasa yanaifanya Afrika kukamilisha idadi ya washiriki 5 katika kombe la dunia ambao ni Misri, Nigeria, Senegal, Tunisia na Morocco.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here