Home Kimataifa Lukaku aondoa ukame wa mabao huku Italia wakiwa mashakani kuelekea Urusi 2018

Lukaku aondoa ukame wa mabao huku Italia wakiwa mashakani kuelekea Urusi 2018

5204
0
SHARE

Timu ya taifa ya Ubelgiji ilikuwa uwanjani usiku wa jana kukabiliana na timu ya taifa ya Mexico ambapo katika mchezo huo Romelu Lukaku alifunga mabao mawili kati ya matatu katika suluhu ya tatu tatu.

Eden Hazard alifunga lingine huku mabao ya Mexico yakipatikana kupitia kwa Andres Guardado aliyefunga kwa penati kabla ya Hirving Lozano kuongeza mengine mawili.

Ufaransa wenyewe walikuwa uwanjani na timu yao inayosadikiwa kuwa ni kizazi cha dhahabu na kuwafunga Wales 2 kwa nunge kupitia kwa Antoine Griezman na Olivier Guroud.

Timu ya taifa ya Ureno nao bila Cr7 walicheza na Saudi Arabia ambapo Ureno waliibuka kidedea kwa mabao 3 kwa nunge mabao ya Ureno yakifungwa na Fernandes, Guedes pamoja na lile la Mario.

Katika hatua ya mtoano kuelekea kombe la dunia timu ya taifa ya Sweden iliishtua Italia baada ya kuwafunga bao 1 kwa nunge na hivyo kuwaweka Italia mashakani kulekea kombe la dunia 2018.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here