Home Kitaifa Julio kalazwa tena ligi daraja la kwanza

Julio kalazwa tena ligi daraja la kwanza

4420
0
SHARE

Dodoma FC imepoteza mechi yake ya pili mfululizo baada ya kufungwa 1-0 na Biashara Mara kwenye mchezo wa leo November 11, 2017 ligi daraja la kwanza Kundi C. Kikosi cha kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kilipoteza mchezo uliopita dhidi ya Pamba ya Mwanza kabla ya kulazwa tena leo.

Matokeo hayo yanaibakisha Dodoma FC na pointi zake 18 ikiachia uongozi wa Kundi C kwa Alliance Schools ambvayo imefikisha pointi 19 baada ya ushindi wake wa leo mabao 4-1 dhidi ya Toto Africans.

Ushindi wa Biashara Mara unafufu matumaini yao ya kucheza ligi kuu Tanzania bara msimu ujao baada ya kufikisha pointi 17 na huku ikiendelea kubaki katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Kundi C pointi moja nyuma ya Dodoma FC yenye pointi 18 katika nafasi ya pili.

Matokeo yote ya mechi za ligi daraja la kwanza zilizochezwa leo November 11, 2017.

Kundi A

  • Mshikamano 3-0 African Lyon
  • Mgambo JKT 0-0 Friend Rangers

Kundi B

  • Mufindi United 0-2 Mbeya Kwanza
  • Polisi Tanzania 2-1 Mawenzi Market

Kundi C

  • Dodoma FC 0-1 Biashara Mara
  • Toto Africans 1-4 Alliance Schools
  • Transit Camp 2-1 Rhino Rangers

Misimamo ya makundi yote (A,B na C) ligi daraja la kwanza

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here