Home Kimataifa Ozil na Sanchez ni nafsi za usaliti kwenye ndoa ya mkeka

Ozil na Sanchez ni nafsi za usaliti kwenye ndoa ya mkeka

3480
0
SHARE

Na Priva ABIUD

Hivi mmesikia alichosema Lee Dixon? Amesema angekuwa yeye ndiye bosi wa Arsenal angeshawatimua Alex Sanchez na Mesut Ozil. Dixon anadai kuwa Fuku fuku hili la Ozil na Sanchez liliwahi kuitokea Arsenal miaka ile 1988 wakiwa Na Mshambuliaji Michael Thomas aliyeifungia Arsenal goli la ushindi kwenye mechi ya fainali dhidi ya liverpool. Inasadikika baada ya goli lile Michael alishikwa tamaa ya maslahi na mwisho wa siku aliuzwa Liverpool.

Lee Dixon anaamini ni bora kuishi na wanajeshi wadhaifu kuliko  mashujaa wanafiki na wenye roho za usaliti kwa sababu ya tamaa. Ozil yupo mbioni kutimka Arsenal kwa taarifa za Maguel Delaney wa The Guardian. Michael Laurence wa whoscored.com amesema Ozil amekuwa akilaumiwa kila mara hasa timu inapokosa matokeo. Mashabiki wa Arsenal wanaamini Ozil kaficha Chenza anawapa machungwa tu. Kwangu Mimi naona mfumo mzima wa Ndoa yake na Arsenal umejengwa na harusi ya mkeka. Ozil akiwa na timu ya taifa kufikia mwaka 2013 alifunga magoli 17 katika michezo 47 akiwa na idadi sawa na ya Karim benzema aliyekuwa na magoli 17 kwenye michezo zaidi ya 50. Kwa sasa ana magoli 22 michezo 86 huku Benzema akiwa na magoli 26 mechi 81. Angalia namna Ozil alifanya vizuri akiwa na timu nzuri.

Mimi bado anamini Ozil na Sanchez wana umuhimu mkubwa, kwa sababu Arsenal haijawahi kushindwa mchezo wowote wa ligi ambao aidha Sanchez na Ozil hawajanza.

Kuna jambo huwa naliwaza sana. Hivi ni kweli Mesut Ozil alikubali kuondoka Madrid na Kwenda Arsenal? Alikosa nini? Kipi kilimsukuma kutoka timu kubwa aliyobeba nayo La liga na kutwaa kikombe cha Copa De la Rey? Je hata kama Madrid ilikuwa hamhitaji je aliona nini Arsenal? Utagundua hapa palikuwepo na ndoa ya mkeka.

Kwa Upande wa Sanchez, akiwa barcelona alianza Michezo 65 huku akitokea benchi michezo 23, lakini alipotua Arsenal alianza michezo 104 na kuanzia benchi mechi 7 tu. Unapata picha gani hapa? Utagundua kilichomlazimisha Sanchez kukimbia nyumbani na kwenda kwenye Maisha ya ndoa ya Arsenal ni hakupata nafasi ya kutosha Barca. Barca waligundua kuwa walikuwa wakitumia kiwango cha Sanchez vibaya. Hivyo ilibidi tu wapate hela kuliko kumweka benchi. 

Ingekuwa uamuzi wa ajabu sana kama Sanchez angekataa kuja timu ambayo ingemfanya kuwa mfalme wao. Cha ajabu Sanchez amejikuta dhahabu jalalani. Hakuna ambaye amegundua kama kwenye jalala la Arsenal ipo lulu ndani yake. Jitihada zake zote zinaishia kupata kipigo cha nguruwe kuzaga zagaa nyumba ya shekh (Buyern 10 2 Arsenal).

Sanchez amegundua hii ni ndoa ya mkeka baada ya kuona kuwa kibosile wake wa zamani anamuhitaji kwa udi na uvumba (Pep Guardiola). Kwa huyu mwanaume wake wa sasa Ozil na mke mwenza Sanchez wanafanyishwa kazi kama Punda. Sanchez Anafanyishwa kazi zote ziwe chafu ana safi (amecheza mechi 104 na mechi 7 akitokea benchi). Hi inaonesha kuwa Sanchez hajioni kama mama mwenye nyumba bali anajikuta yeye ni beki tatu. Sura ya Sanchez inaongea kwa sauti kuliko hata mdomo wake. Sanchez sio mtu wa maneno sana hasa ukizingatia lugha n.k . Sanchez mara kadhaa ameonekana uso wake unakaribia kuchakaa kwa kuwa na huzuni ya vipigo vya ajabu ajabu kila mara licha ya jitihada zake. Kuna mechi dhidi ya Buyern Uzalendo ulimshinda ilibidi acheke, hata kama ni wewe ungefanyaje? Kumi kwa mbili?

Akiangalia Mashariki hamuoni shetani, Magharibi haoni malaika, kusini hamuon mwanadamu ila kaskazini  anaona giza.

Roho za Sanchez na Ozil zimeshaisaliti Arsenal lakini naamini ifikapo 2018 tutaona mashekh wa Man City wakienda kutoa talaka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here