Home Kitaifa Mtanzania aliyetangaza fainali ya UEFA 2006 huku analia kwa sababu ya Arsenal

Mtanzania aliyetangaza fainali ya UEFA 2006 huku analia kwa sababu ya Arsenal

9821
0
SHARE

Mtangazaji mkongwe wa soka nchini Juma Nkamia mezitaja mechi tatu ambazo anazikumbuka zaidi katika kipindi chake chote alichokuwa akitangaza soka.

Kubwa kuliko zote ni mechi ya fainali ya michuano ya vilabu bingwa Ulaya mwaka 2006 kati ya Arsenal dhidi ya Barcelona ambapo alitangaza mchezo huo huku akitokwa na machozi baada ya kushuhudia timu anayoipenda (Arsenal) ikiwa nyuma kwa mabao 2-1 huku wachezaji wakiwa pungufu uwanjani kufuatia golikipa Jens Lehmann kuoneshwa kadi nyekundu.

“Mechi ambayo naikumbuka sana ilikuwa kati ya Arsenal na Barcelona iliyochezwa Stade de France Paris (fainali ya vilabu bingwa Ulaya 2006) mechi ambayo Arsenal walifungwa 2-1, nakumbuka goli la pili lilifungwa na Samuel Eto’o Fils.”

“Ni mechi ambayo Jens Lehmann alioneshwa kadi nyekundu, mimi ni shabiki wa Arsenal kwa hiyo mechi hiyo naikumbuka nilikuwa tangaza hadi machozi yananitoka, ni mambo ambayo nayakumbuka sana.”

Mchezo mwingine ambao bado upo kwenye kumbukumbu za Nkamia ni ule wa AFC Leopard vs Simba katika mashindano ya vilabu bingwa Afrika uliochezwa jijini Nairobi Kenya.

“Nakumbuka mchezo kati ya Simba dhidi ya AFC Leopards ilikuwa ni michuano ya East & Central Afrika pale Nairobi, ilikuwa ni mwezi wa Ramadhani (mwezi mtukufu0 nilikuwa natangaza mechi mbili kwa siku kwa sababu nilikuwa pekeangu.”

Mechi nyingine ambayo Nkamia anaikumbuka sana ni kati ya Express ya Uganda vs Yanga kwa sababu aliingiza mkwanja bila kutegemea kutoka kwa mtangazaji mwenzake.

“Nakumbuka nilikutana na mtangazaji mmoja wa Kenya anaitwa Leonard Mambo Mbotela alikuja akanikuta naandika majina ya wachezaji (lineups) akaniuliza, mtangazaji yupo wapi? kwa sababu nilikuwa bado kijana mdogo sana nikamwambia yupo chini anachukua majina ya wachezaji.”

“Badae akaja akanikuta natangaza hakuamini kama ni mimi akanipa shilingi 20,000 ya Kenya. hiyo mechi naikumbuka sana na Simba ilifungwa 2-1.”

“Naikumbuka mechi kati ya Yanga na Express, mechi ambayo ilichezwa uwanja wa Nakivubo pale Kampala ilimalizika kwa sare ilikuwa michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika.”

Kama ulikuwa hujui basi chukua hii, Juma Nkamia ndio mtangazaji wa kwanza kutangaza ligi ya England (EPL) na ligi ya Ulaya (UEFA Champions League) kwa kiswahili pale BBC.

Kwa sasa Nkamia anajihusisha na mambo ya siasa akiwa ni mbunge wa jimbo la Chemba (CCM), hajasikika kwa muda mrefu katika fani yake ya utangazaji soka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here