Home Ligi EPL Kwanini itakuwa Guardiola na Man City kumaliza msimu bila kufungwa

Kwanini itakuwa Guardiola na Man City kumaliza msimu bila kufungwa

7493
0
SHARE

Hawazuiliki, hawashindiki, hawafungiki – hivi ndivyo wanavyoelezewa Manchester City msimu huu.

City wameanza msimu na moto wa gesi, wakiweka rekodi za kila aina. Wamekuwa timu ya pili kuanza ligi kwa mafanikio haya katika historia tangu Spurs walipoanza kwa kushinda mechi 11 msimu wa 1960-61. Kwa mwendo kama Utaendelea hivi mpaka mwishoni mwa msimu basi huenda wakamaliza na pointi 107 na magoli 133. Kiwango chap kimeleta maswali kama kuna timu yoyote itakayoweza kuwasimamisha ndani ya dakika 90 au ndani ya mechi 38.

“Kama wataendelea kupata upendeleo wa maamuzi katika uwanja wa nyumbani namna hii, basi hakuna atakayeweza kuwazuia,” alisema Arsene Wenger, akizungumza kwa hasira kuhusu goli la penati na lile alilofunga Jesus katika kipigo cha 3-1 Jumapili iliyopita.

Hata hivyo historia inatumbia kwamba kuna mahala City watakwama wakati msimu ukiendelea, sio tu kwasababu bado hawajakutanana wapinzani wao wakubwa kwenye mbio za ubingwa: Tottenham Hotspur na Manchester United lakini pia kadri msimu unavyoenda ipo siku watasimamishwa.

Kuna sababu maalum kwanini naamini watasimamishwa: Tayari wanamchezesha kiungo kwenye safu ya ulinzi wa kushoto kwasababu Benjamin Mendy amepata majeraha yatakayomuweka nje kwa muda mrefu, Fabian Delph anafanya kazi nzuri, lakini itatokea wakati wapinzani watautumia udhaifu wake.

Ikitokea akapata majeruhi kutokana na historia yake ya kuumia mara kwa mara basi Pep itabidi atafute mbadala wa 3.

Upande wa ulinzi wa kati – wana uimara wa kutosha? Huku Vincent Kompany akiwa nje kwa majeruhi, Nicolas Otamendi akiwa kifungobi katika mchezo ujao vs Leicester, Eliaquim Mangala anategemewa kuchukua nafasi. Endapo City watapata majeruhi mmoja katika safu ya kati ya ulinzi, mfaransa huyu ambaye alicheza hovyo vs Wolves katika Carabao Cup, ataanza kupewa nafasi mara nyingi zaidi kikosini. Hata Otamendi ambaye msimu huu ameimarika, bado ana makosa mengi. Alinyanyaswa mno na Mohamed Salah kwa dakika 45 mnamo September. Golini, endapo Ederson ataumia itabidi wamrudishe Bravo.

City wana uimara zaidi katika nafasi 6 za mbele ya uwanja, lakini hakuna mbadala sahihi wa Fernandinho katika kikosi chao. Hakuna anayeweza kuziba vizuri pengo la Kevin de Bruyne na mchango anaoutoa kwenye timu. Yoyote kati yao akipata majeruhi City watakuwa na udhaifu mkubwa katikati katika kuucheza mchezo ambao wameuzoea na unaowapa sifa kubwa katika dunia ya soka. Wakati City walipocheza na Wolves, De Bruyne na Fernandinho hawakuanza na City wakapoteza unyumbulifu wao na hawakucheza mchezo wao na matokeo yake mchezo ukaenda mpaka dakika ya 120.

Halafu kuna sababu za ujumla kwanini timu yoyote inaweza kupata taabu kupata matokeo: wanaweza kucheza dhidi ya wapinzani ambao golikipa wao anaweza kuwa kwenye kiwango cha aina yake, na pia wakati mwingine maamuzi ya refa au timu pinzani ikawa na bahati zaidi yao.

Na ndio maana ni ngumu sana kwa City kumaliza msimu bila kupoteza. “Ipo timu itakuja kutufunga,” Guardiola alisema Ijumaa iliyopita. Ukweli wa kwamba kikosi cha Wenger cha msimu wa 2003-04 ndio kikosi cha mwisho kumaliza ligi bila kupoteza inaonyesha wazi namna jambo hilo lilivyo gumu. Hii suala halikutakiwa kuanza kuongelewa kabla hata January.

Spurs walianza ligi kupoteza kwa muda mrefu msimu uliopita, Chelsea pia msimu wa 2014-15, City wenyewe pia msimu wa 2012-13 na Liverpool 2007-08. Ni timu moja kati ya hizo ndio ilienda kutwaa ubingwa. Kuna timu ambazo zilianza ligi bila kupoteza kwa muda mrefu huko nyuma na baadae wakaenda kuchukua ubingwa lakini hawakufanikiwa hata kusogelea kumaliza ligi bila kufungwa:

Manchester United hawakupoteza mechi 24 za mwanzo wa ligi msimu wa 2010-11, Liverpool katika mechi 29 za mwanzo 1987-88 au Leeds katika mechi 29 msimu wa 1973-74, wote wakaishia kufungwa mara 4 mpaka kufikia mwishoni mwa misimu hiyo.

Mpaka sasa City wapo mbele kwa pointi 8. Guardiola akasema bado kuna pointi 84 za kushindania, sasa zimepungua mpaka 81 baada ya ushindi wikiendi iliyopita. Lakini miaka 8 iliyopita, kikosi cha United ambacho kilishinda makombe ya ligi 4 katika misimu 5 ya nyuma, kilikuwa mbele kwa pointi 8 mbele huku mechi 6 zikiwa zimebakia. City wakaenda wakabeba ndoo.

Ndio maana haishangazi Jose Mourinho alisema Jumapili iliyopita faida ya kuongoza kwa pointi 8 katika EPL sio sawa na ile ya ligi kama za Ureno, La Liga, au Bundesliga. “Sio pengo ambalo huenda likashindikana kulifikia hapa England. Real Madrid hawajawahi kutoka nyuma kwa pointi na kwenda kushinda ubingwa; United walishawahi kutoka nyuma kwa tofauti ya pointi 12 nyuma ya Newcastle msimu wa 1995/96 na wakachukua ubingwa”. Miaka 3 iliyopita, Chelsea ya Mourinho walikuwa mbele kwa pengo la pointi 8 mbele ya City ya Pellegrini, City wakalifuta pengo hilo na kuwafikia Chelsea kabla ya The Blues kufanikiwa kuwazidi mwishoni na kutwaa ubingwa.

Yote haya hayawezi kuondoa ukweli kuhusu ubora wa City, wamekuwa ndio timu bora, yenye kufunga magoli mengi na inayocheza soka la kuvutia zaidi. Lakini kufanikiwa mwanzoni mwa msimu ni mbali sana na suala kutokufungika hasa kwenye ligi ya England.

City wameshawahi kuanza hivi ligi msimu wa 2011-12, wakishinda mechi 10 katika mechi 11 za kwanza na wakifunga goli 1 zaidi ya idadi ya sasa, lakini walienda mpaka mwishoni mwa msimu wakiwa wameshapoteza mechi 5. Walitegemea goli la maajabu la dakika ya 94 ya mchezo wa mwisho kufanikiwa kuwa mabingwa kwa tofauti ya magoli.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here