Home Kimataifa Carzola anaamini pilipili ni tamu kuliko sukari

Carzola anaamini pilipili ni tamu kuliko sukari

4467
0
SHARE

Na Privaldinho ABIUD

Hivi unadhani Carzola anajisikiaje pale India Ursula akimuuliza baba mbona huendi kazini? Katikati mwa msimu jibu rahisi la Carzola Kwa Mwanae lilikuwa “mwanangi nitarudi kazini mwezi wa kumi” 

Mwezi wa kumi umefika na Carzola bado hajarudi kazini. Swali gumu zaidi kwa mwanae ni “baba mbona kwenye picha ya pamoja ya Arsenal ya Msimu hu haupo? Carzola itabidi amwambie nitarudi kazin mwakani. 

Michael Owen aliteseka na Majeruhi maisha yake yote ya soka. Alipofika mwaka 2013 aliona bora awe Dr Leakey wa England ili acheze mpira wa mdomoni kwenye vituo vya Tv baada ya Mateso ya misuli kwa kipindi kirefu. Mwaka 2007 Dr Richard Steadman alimweleza Ji sung Park kuwa opereshen yake ya goti itamweka benchi mwaka mmoja, haikuwa taarifa nzuri. 

Huyu Dr maarufu aliwahi kuwatibu akina Ronaldo, Ruud van Nistelrooy, Michael Owen na Alan Sheare na kuwaeleza wazi kuwa matatizo yao ya misuli yatahitimisha soka lao.Carzola nae tokea mwezi wa 10 mwaka jana hayupo uwanjani. Dr wake ndugu Roman Cugat huenda ndiye mwenye majibu sahihi kwa mtoto wa Carzola ambaye anamuuliza baba kwanini huendi kazini. Jibu la Cugat kwa mtoto wa Carzola ni moja tu. Amweke wazi kama Steadman alivyofanya kwa akina Delima. Amweleze ukweli kuwa baba hawezi kurudi uwanjani mapema hivyo atarudi Lugo de Llanera in Oviedo (nyumbani kwao).

Michael Owen aliumia mnamo tar 12 mwezi wa 4 mwaka 1992 akiwa na Liverpool kule Leeds. Mwaka 2007 alikaa nje ya uwanja takriban siku 315. Achana na 2012 ambapo alikaa nje kwa siki 129. Maisha haya ya Owen kushindwa kuishi kwa amani ndiyo yanamrudisha Carzola Llanera. Wakazi wa Asturias walizoea kumuona Carzola akikatiza misitu ya akina Vidic, Terry na Cahil. Wamemisi kumuona Carzola akimpa Furaha Wenger. 

Dr wake Roman Cugat ameshauri Carzola aachane na soka. Huu ni uamuzi mgumu sana kwake. Tokea mwezi wa 10 mwaka jana ilisemekana Carzola atatumia siku 346 akiwa benchi. Lakini kutokuwepo kwa Carzola kwenge picha ya pamoja ya Arsenal msimu huu basi huenda asiwepo mpaka mwakani. 

Ana umri wa miaka 32 kwa sasa, unategemea nini?

Ingawa Carzola Bado anaamini kuwa pilipili ni tamu kuliko sukari, ana Imani na misuli yake kuwa ina uwezo wakupambana majira yote.

Ndani ya miaka 8, Carzola amelitumikia benchi siku 608. Takribani miaka miwili amekuwa akitembea na magongo. Bila shaka  uhakika wa namba nane kwa Carzola itakuwa uwongo, misuli ya Carzola itaanza ushindani na Granit Xhaka. Nje yupo Ramsey, pia yupo Elneny. Usisahau kuwa Ozil atasimama kama namba 10.

Chumba cha Carzola ni kama kimeshanunuliwa. 

Mashabiki wa Arsenal watatamani kunirushia mawe, lakini niwaambieni tu ukweli, tafuteni video za Falcao aliyetokea benchi baada ya kukaa miezi 8 alikuwa na hali gani.

Labda tu tujiulize unafikiri swali la Enzo (mtoto wa Carzola) linampa hisia gani?

Kwa upande wangu huu ni wakati wa yeye kupunguza ruti za hospitali kila siku. Kiasi cha pesa alichokitumia kwenye upasuaji nadhani ni vyema arudi Cimavilla na fukwe za Abba Kaya kule Gijon akapunge upepo na mke wake Ursula. Aliyoyafanya ni makubwa. Asijikute Fransesco Totti. Misuli yake na akili vinaandamwa kama ishu ya makinikia.

Carzola amewekeza sehemu nyingi mno. Mwaka 2014 aliwekeza kwenye kampuni ya ardhi na makazi yenye ofisi zake Liverpool na Man United ijulikanayo kama Capital Centric Investments LLP. Ambapo yeye na Luis Suarez, Mikel Arteta na Jose Henrique waliwekeza zaidi ya Euro milioni 50 na wanategemea kupata faida ya sio chini ya Euro 250 milioni kwa mwaka. Wote walikuwa wakurugenzi kwenye kampuni moja licha ya uhasama wao wa kitimu wakiwa pamoja na akina Higgins. 

Nadhani huu ni wakati wa yeye kusimamia mambo yake Mengine ya kibiashara pamoja na wa ubavu wake. Amebarikiwa kuwa na mwanamke msomi waliyetokea nae kijiji kimoja. Mke wake huyu ni msomi mkubwa tu. Ana Degree ya   sayansi ya elimu ya viungo. Ni muda muafaka wa yeye kuwekeza zaidi na kufanya mambo mengine.. ni ngumu kukubali lakini sijui kama kuna namna ya Carzola ambaye muda sio mrefu atafikisha miaka 34 kurudi katika ubora wake. Kila la kheri kwake na nampa pole pia…

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here