Home Kimataifa Alvaro Morata akaribia kuifikia rekodi ya Jose Mourinho

Alvaro Morata akaribia kuifikia rekodi ya Jose Mourinho

6353
0
SHARE

Hadi hivi sasa Jose Mourinho ndio kocha ambaye ana mafanikio katika ligi tatu kubwa barani Ulaya. Ligi za Serie A, La Liga na Epl ambazo Mourinho alifundisha alifanikiwa kubeba makombe.

Lakini hivi sasa mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Hispania Alvaro Morata anaonekana kutaka kufanya kile ambacho kocha Jose Mourinho ameshakifanya katika ligi alizozipitia.

Tayari Alvaro Morata ameshabeba ubingwa wa Serie A akiwa na Juventus na msimu uliopita alikuwepo katika kikosi cha Realadrid kilichotwaa ubingea wa michuano ya Champions League na La Liga.

Kwa sasa Alvaro Morata yuko Chelsea ambako nako kama akipata ubingwa wa Uingereza baasi atafikia rekodi ya Mourinho ya kubeba mataji katika ligi kuu tatu kubwa barani Ulaya.

Alvaro Morata mwenyewe amekiri kufurahia kuwa Chelsea na kusema kwamba hajutii uhamisho huo kwani unamfundisha kitu kipya huku pia akiwa na malengo ya kufanya alichofanya Hispania na Italia.

Morata sio mchezaji wa kwanza kucheza Serie A, La Liga na Epl kwani wapo wakina Pepe Reina, Fernando Torres, Gaizka Mandite na Michu lakini kati yao hakuna aliyefanikiwa kuchukua kombe kwenye nchi zote tatu.

Alvaro Morata alikuwa shujaa wiki iliyopita akifunga bao pekee lililoiua Manchester United na kuwafanya Chelsea kupunguza pengo la alama kati yao na Manchester United hadi kufikia tofauti ya alama moja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here