Home Kitaifa Muuaji wa Yanga kaitwa Zanzibar Heroes

Muuaji wa Yanga kaitwa Zanzibar Heroes

7478
0
SHARE

Na Abubakar Khatib ‘Kisandu’, Zanzibar

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Hemed Suleiman ‘Morocco’ amemuongeza kwenye kikosi Mshambuliaji wa Lipuli ya Iringa Seif Rashid Abdallah ‘Karihe’ ili kuzidi kuipa nguvu timu hiyo itakayokwenda Kenya katika Mashindano ya CECAFA Challenge Cup yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 na kumalizika Disemba 9, 2017.

Karihe ndio mchezaji wa kwanza kufunga goli dhidi ya Yanga msimu huu kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara ambapo alifunga bao kwenye mechi yao ya ufunguzi wa msimu huu August 27, 2017 Yanga lipotoka sare ya kufungana 1-1 na Lipuli kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.

Katika uteuzi wa awali wa wachezaji 30 Karihe hakuitwa lakini kocha Morocco amelazimika kumuongeza mshambuliaji huyo na atakuwa mchezaji wa 31 kuitwa katika kikosi cha awali huku Morocco akisema si kosa kwa timu ya Taifa kupunguza au kuongeza mchezaji wakati wowote tu ikiwa bado haijaenda katika Mashindano.

“Hii ni timu ya Taifa wakati wowote unamwita mchezaji au unamtoa kutokana na mahitaji yako, nimelazimika kumuongeza Karihe kwasasa ataungana na wenzake 30 wale wa awali”- Morocco.

Karihe ambae ni mchezaji wa zamani wa Azam FC ataungana na wenzake Ahmed Ali ‘Salula’ (Taifa ya Jang’ombe), Nassor Mrisho (Okapi), Mohammed Abdulrahman ‘Wawesha’ (JKU), Abdallah Haji ‘Ninja’ (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed ‘Sangula’ (Jang’ombe Boys), Adeyum Saleh ‘Machupa’ (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abubakar Ame ‘Luiz’ (Mlandege), Issa Haidar ‘Mwalala’ (JKU),  Abdulla Kheir ‘Sebo’ (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang’ombe).

Wengine ni Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang’ombe), Mudathir Yahya (Singida United), Omar Juma ‘Zimbwe’ (Chipukizi), Mohd Issa ‘Banka’ (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman ‘Pwina’ (JKU), Mbarouk Marshed (Super Falcon), Ali Yahya (Academy Spain), Hamad Mshamata (Chuoni), Suleiman Kassim ‘Selembe’ (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons), Matteo Anton (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang’ombe), Feisal Salum (JKU), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa ‘Rais’ (Jang’ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here