Home Ligi EPL Cazorla: Hivi ndivyo majeruhi yalivyotishia ndoto yangu, upasuaji mara 8, almanusra kukatwa...

Cazorla: Hivi ndivyo majeruhi yalivyotishia ndoto yangu, upasuaji mara 8, almanusra kukatwa mguu

9783
0
SHARE

Ukubwa wa majeruhi ya muda ya Santi Cazorla unaelezewa na mchezaji mwenyewe ambaye aliambiwa na madaktari kwamba akiweza tu kutembea na mwanae kwenye bustani basi yangekuwa ni mafanikio makubwa.

Ilikuwa mnamo September 10, 2013 jijini Geneva wakati Spain wakicheza mechi ya kirafiki na Chile, Cazorla akashindwa kumaliza mchezo baada ya kutokana na kuumia enka, jeraha ambalo liliacha mpasuko kwenye mfupa. Tangu wakati huo, alijifunza kuishi na kucheza na maumivu katika mguu wake wa kulia.

Picha inayoonyesha namna mguu wake wa kulia ulivyorika baada ya upasuaji

“Mara ya kwanza nilikuwa naweza kuvumilia maumivu kiasi kidogo. Nilikuwa nikipata joto kidogo nilikuwa naweza kucheza, lakini ilipofika wakati wa mapumziko na mwili ukishapoa nilikuwa napata maumivu ambayo nilikuwa naishia kutoa machozi.”

December 5, 2015, alifanyiwa upasuaji kutoka na kuumia goti la kushoto, lakini tatizo la kwenye enka liliendelea kukua.

Lakini kutokana na matamanio yake ya mchezaji muhimu katika kikosi cha Arsenal, aliendelea kujaribu kuvumilia kadri alivyoweza lakini hakukuwa na namna zaidi kupata matibabu.

Mpaka kufikia hatua hiyo, Cazorla hakuweza kufikiria kwamba njia yake ya matibabu ingekuwa ndefu na nyeusi, kwa kufanyiwa upasuaji mmoja baada ya mwingine.

Madaktari nchini Uingereza hawakuwa wakimpa imani vya kutosha.

“Ikitokea umeweza kutembea tena hata mwanao kwenye bustani, basi ridhik, walianiambia hivyo madaktari.” – anasema Cazorla.

Hivyo soka Ilibidi lilirudi siti ya nyuma na kuweka umakini wote kwenye kupona majeraha na angalau aweze hata kutembe tena.

Mwaka mmoja baada ya upasuaji kwenye goti, akahitaji upasuaji mwingine kwene msuli wa paja wa mguu wa kulia.

Picha inaonyesha jeraha la enka kwenye mfupa wa ndani kabisa

Kile kilichoonekana kitamuweka nje kwa wiki 3, kilitishia kumaliza maisha yako soka ya Cazorla.

Baada ya mwezi upasuaji wa enka, nyuzi zikaondolewa, lakini kidonda kikawa kinafunguka kila kukicha, ilifikia hatua ikabidi afanyiwe upasuaji mara 8 zaidi ndani ya mwaka.

Kuna wakati kipindi hicho bado nilikuwa nacheza. Wataalam waliniambia haikuwa na shida, tatizo lilikuwa kwamba kidonda hakikupona na kikawa kinafunguka mara kwa mara, kilipata maambuziki.”

Hakuweza kufikiria ambacho alikuja kuambiwa na Dr. Mikel Sanchez alipokutana nae huko Vitoria mnamo May 2017.

Cazorla alikutana na daktari huyo baada ya kukosa tiba nchini England.

Akiwa chumba cha upasuaji Dr Sanchez alimwambia maneno ambayo yalimfanya ashike kichwa.

Aliona jinsi maambukizi yalivyo makubwa, na jinsi mifupa ilivyorika.” Cazorla anaelezea.

“Kulikuwa na shimo kubwa, angalau sentimenta 8 za mfupa zilikuwa zimepotea kuingia ndani.”

Wakati huo ndio waligundua wadudu wengine wa bacteria ambao walikuwa wanashambulia kwa kasi mfupa, na kuzidisha maambukizi..

Cazorla alifanyiwa matibabu kadhaa yaliyofanikiwa ya antibiotic lakini kulikuwa na tishio kwamba maambukizi ya damu yangeweza kukatwa kwa mguu.

Dr. Sanchez mwenyewe, ambaye alikiri kwamba hakuwahi kuona tatizo la namna hiyo, alimfanyoa upasuaji wa mwisho mnamo May 29.

Wakati wa kiangazi uliopita Cazorla akaanza program ya rehabilitation na amekuwa akiendelea vizuri.

Hivi sasa ute ute wa mifupa umepunguza kasi ya uponaji, lakini pia mpai sasa haijafahamika atarudi lini uwanjani.

Arsenal wameshaongeza mkataba mnamo November 2017 mpaka June 2018, na anataka kurudi uwanjani kucheza tena soka.

“Sina ruhusa ya kucheza mpaka January, lakini nitarudi wakati huo ukifika.”

Mwezi mmoja uliopita alikuwa akikimbia kwenye uwanja wa Estadio Helmantico na kaka yake alipomuona alianza kutokwa na machozi.

Tangu July, Cazorla amekuwa akiishi hotelini katik jiji la Salamanca akipatiwa matibabu.

“Familia yangu ipo London kwa sababu watoto wangu walianza shule kule. Kuwa hapa mwenyewe bila uwepo wao ni kitu kigumu sana kwangu.”

Kila asubuhi anaamka mapema na kuanza mazoezi kwenye swimming, anatumia lisaa limoja kwenye baiskeli kila siku kwenye mazoezi yake.

“Mara nyingi sana anapokea message za kunitakia kheri kutoka Iniesta, Silva, Villa… ,” anasema, huku akikumbuka mafanikio ya kushinda ubingwa wa ulaya mara mbili.

Anasema hakujitaji kupata mwanasaikolojia kwa ajili ya kumuongoza katika kipindi hiki kigumu alichopopitia.

“Namshukuru Mungu kwa kila kitu, yote niliyopitia hayakuwa rahisi – halikuwa tu jeraha la kawaida kama watu walivyoamini. ‘Hakuna aliyeamini nitarudi uwanjani, ila nashukuru sasa naendelea vyema sana, NITAREJEA tena uwanjani.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here