Home Kitaifa Siku 176 zimepita tangu Ruvu Shooting ipate ushindi wa mwisho VPL

Siku 176 zimepita tangu Ruvu Shooting ipate ushindi wa mwisho VPL

2174
0
SHARE

Ruvu Shooting ndio timu pekee ya ligi kuu Tanzania bara ambayo bado haijashinda hata mechi moja tangu kuanza kwa msimu huu (2017/2018) ikiwa tayari kila timu imecheza mechi tisa hadi sasa.

Kikosi hicho cha kocha Abdulmutik Haji akisaidiwa na Selemani Mtungwe kimepoteza mechi nne na kutoka sare katika mechi zake tano, imekusanya pointi tano sawa na idadi ya mechi zake ilizotoka sare.

Ruvu Shooting ndio timu iliyofungwa magoli mengi zaidi, imeshafungwa magoli 14 tangu ligi ilivyoanza msimu huu huku yenyewe ikiwa imefunga magoli matatu na kufanya wastani wake wa magoli kuwa -11.

Mara ya mwisho Ruvu Shooting kupata ushindi ilikuwa May 14, 2017 msimu uliopita (2016/17)  ilipoifunga African Lyon  1-0 kwenye uwanja wa Uhuru Dar baada ya hapo ilipoteza mchezo wake wa mwisho msimu uliopita kwa kufungwa na 2-1 na Stand United kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga. Tangu hapo matokeo ya vipigo na sare yamekuwa rafiki kwa Ruvu Shooting.

Matokeo ya Ruvu Shooting msimu huu 2017/2018

  • 26/08/2017 Simba 7-0 Ruvu Shooting
  • 10/09/2017 Kagera Sugar 1-1 Ruvu Shooting
  • 16/09/2017 Lipuli 0-0 Ruvu Shooting
  • 24/09/2017 Ruvu Shooting 1-1 Mtibwa Sugar
  • 30/09/2017 Ruvu Shooting 1-1 Njombe Mji
  • 14/10/2017 Ruvu Shooting 0-0 Singida United
  • 21/10/ 2017 Mbeya City 2-0 Ruvu Shooting
  • 30/10/2017 Tanzania Prisons 1-0 Ruvu Shooting
  • 04/11/2017 Azam 1-0 Ruvu Shooting

Baada ya kufungwa 7-0 na Simba kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi msimu huu, Ruvu Shooting ilitoka sare katika mechi tano mfululizo zilizofuata, baada ya hapo ikapoteza mechi tatu mfululizo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here