Home Kitaifa Mkufunzi wa waamuzi CAF apata kigugumizi goli la Kichuya vs Mbeya City

Mkufunzi wa waamuzi CAF apata kigugumizi goli la Kichuya vs Mbeya City

19592
0
SHARE

Goli alilofunga Shiza Kichuya kwenye mchezo wa VPL kati ya Mbeya City dhidi ya Simba limezua mjada mkubwa kwa wadau wa soka wapo wanaosema kabla Kichuya hajapokea pasi kutoka kwa Jonas Mkude alikuwa ameotea (Offside) huku wengine wakisema hakuwa ameotea (alikuwa-Onside).  Kila mtu amekuwa akiamini kile anachokiamini kutokana na utata uliopo kabla ya goli hilo kufungwa.

Mkufunzi wa waamuzi anayetambuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Leslie Liunda kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa kitaalamu zaidi lakini katika maoni yake ameshindwa kusema moja kwa moja kama Kichuya alikuwa offside au onside kabla ya kufunga goli.

“Kamera hazikuonesha vyema, offside inaamuliwa wakati mpira unapigwa si wakati wa kupokea mpira. Picha haioneshi vizuri wakati mpira unapigwa nafasi ya Kichuya ilikuwaje, hivyo tunapaswa kukubaliana na maamuzi ya mwamuzi msaidizi (assistant referee)”- ) Leslie Liunda.

Ukiachana na mazingira ambayo Kichya alifunga goli (yanatajwa kuwa tata) mjadala mwingine unaoendelea ni kuhusu mpira ulioguswa kwa mkono na Jonas Mkudeakiwa kwenye eneo la penati, wapo wanaoamini kwamba mwamuzi alitakiwa kutoa adhabu ya mkwaju wa penati kutokana na kitendo cha Mkude kuushika mpira lakini wapo wengine wanasema mpira ulifuata mkono.

Nipe maoni yako (unachokiamini wewe) kutokana na matukio hayo mawili yaliyotokea kwenye mchezo wa jana Jumapili November 5, 2017 mechi iliyomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here