Home Kitaifa Yanga yashukuru kuambulia angalau pointi moja Singida

Yanga yashukuru kuambulia angalau pointi moja Singida

5967
0
SHARE

Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amesema wamepokea kwa mikono miwili pointi moja waliyoipata ugenini kwenye uwanja wa Namfua baada ya kulazimishwa suluhu na Singida United kwenye mechi yao ya VPL raundi ya tisa.

Nsajigwa amesema, lengo la Yanga lilikuwa ni kupata ushindi lakini wanashukuru kupata pointi moja ugenini, amekiri kwamba timu yake ilibanwa kipindi cha kwanza, kama wachezaji wa Singida United wangetulia wangeweza kupata bao la kuongoza.

“Kuanzia kipindi cha kwanza Singida walijitahidi na walitengeneza nafasi, nadhani hawakutulia wangeweza kuongoza, kipindi cha kwanza hichohicho baadae mchezo ukawa 50/50. Kipindi cha pili kilianza Singida United wakiwa vizuri lakibi baadae kidogo na sisi tukatawala ikawa sisi kidogo leo hatuwa kwenye hali yetu ya kawaida lakini kikubwa tunashukuru tumepata pointi moja ugenini licha ya kuhitaji ushindi kama lilivyokuwa lengo letu.”

“Upepo kwa kiasi fulani ulikuwa kikwazo lakini sio kisingizio kikubwa kwa sababu hata Singida wenyewe walikuwa wanacheza hapa kwa hiyo kiufundi Singida kipindi cha kwanza walicheza vizuri na kutengeneza nafasi na sisi kipindi cha pili angalau tumepata nafasi moja au mbili.”

Baada ya matokeo ya suluhu dhidi ya Singida United, kikosi cha Yanga kimefikisha pointi 17 sawa na Mtibwa Sugar lakini Yanga inabaki katika nafasi ya pili kutokana na wastani wa magoli nyuma ya Azam wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 19 huku ikisubiriwa mechi ya Mbeya City vs Simba kuamua timu itakayoongoza ligi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here