Home Kitaifa “Tumetengeneza nafasi 3 tumeshindwa kufunga”, kocha wa Singida kataja sababu za Yanga...

“Tumetengeneza nafasi 3 tumeshindwa kufunga”, kocha wa Singida kataja sababu za Yanga kutoka salama Namfua

4323
0
SHARE

Licha ya kutawala mechi kwa asilimia nyingi, kikosi cha Singida United hakikufanikiwa fufunga bao kwenye mechi yao ya kwanza kwenye uwanja wa Namfua msimu huu walipocheza na Yanga katika mchezo wa VPL raundi ya tisa, sababu kubwa ya kikosi cha Hans van Pluijm kushindwa kufunga inatajwa ni ubutu wa safu yao ya ushambuliaji.

Kocha msaidizi wa Singida United Jumanne Chale amekiri safu yao ya ushambuliaji ni tatizo kwao kwa sababu  wamecheza mfululizo bila kufunga.

“Mpira ulikuwa wa kasi sana lakini tumepata sare kwa sababu ndio kwanza tumeukanyaga uwanja wa Singida kuambulia sare pia sio kitu kibaya kwetu, wachezaji wetu wamecheza vizuri tumetengeneza nafasi kama tatu tumepoteza basi kwa hiyo sare kwetu sio mbaya.”

“Nadhani sehemu ya ushambuliaji ambapo hadi sasa tumecheza mechi tatu nje tumetoka sare za bila kufungana ina maana kuna matatizo katika sehemu ya ushambuliaji ambayo sasa hivi ndio tunajaribu kushughulika nayo.”

Hadi sasa Singida United imecheza mechi nne mfululizo bila kufunga goli sawa na dakika 360, lakini pia katika dakika hizo, timu hiyo haijaruhusu kufungwa goli.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here