Home Kitaifa Singida United imezindua uwanja kwa kuibana Yanga

Singida United imezindua uwanja kwa kuibana Yanga

2709
0
SHARE

Ikicheza kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wake wa nyumbani Namfua Stadium, Singida United imeibana Yanga baada timu hizo kutoka suluhu kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Singida United ilikuwa ikiutumia uwanja wa Jamhuri Dodoma kama uwanja wao wa nyumbani wakipisha matengenezo makubwa ya uwanja wa Namfua ili ukidhi vigezo vya kutumika katika michezo ya ligi kuu.

Mashabiki wa soka mkoa wa Singida na maeneo ya jirani walijitokeza kwa wingi kuhudia mchezo huu, tiketi zilianza kuuzwa asubuhi na mapema hadi kufikia saa 6 mchana majukwaa ya uwanja yalikuwa yamejaa hivyo mashabiki kulazimika kusimama.

Singida United walifanikiwa kuibana Yanga na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umakini kwenye umaliziaji ndio umewanyima ushindi katika mchezo huo.

  • Yanga imefikisha pointi 17 na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa inalingana kwa pointi na Mtibwa Sugar ambayo pia imetoka sare dhidi ya Ndanda, hivyo timu hizo mbili zinatofautiana wastani wa magoli zikiwa zimeshacheza mechi tisa, baada ya Azam kushinda 1-0 vs Ruvu Shooting wamefikisha pointi 19 na kuongoza msimamo wa ligi huku matokeo ya Mbeya City vs Simba (kesho) yataamua timu gani itaongoza ligi baada ya mechi za mwisho wa juma hili.

  • Baada ya sare ya kufungana 1-1 kwenye mchezo uliopita dhidi ya Simba, kwa mara ya kwanza ndani ya msimu huu Yanga imepata sare kwenye mechi mbili mfululizo. Ni sare ya tano kwa upande wa Yanga tangu kuanza kwa ligi msimu huu lakini ni ya pili kwa mechi zao za ugenini.

  • Singida United imefikisha pointi 14 baada ya sare yake dhidi ya Yanga na imeporomoka kutoka nafasi ya sita hadi nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi.

  • Singinda United imefikisha mechi tano bila kupata ushindi, sare dhidi ya Yanga ni ya tano mfululizo, ushindi wao wa mwisho ulikuwa ni September 24, 2017 walipoifunga Kagera Sugar 1-0 kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa leo November 4, 2017

  • Kagera Sugar 1-1 Prisons
  • Njombe Mji 0-0 Mbao
  • Azam 1-0 Ruvu Shooting
  • Ndanda 0-0 Mtibwa Sugar

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here