Home Ligi EPL Chelsea vs Man United: Mourinho kuumaliza uteja wa United Darajani?

Chelsea vs Man United: Mourinho kuumaliza uteja wa United Darajani?

6375
0
SHARE

Chelsea na Manchester United wanaingia katika mchezo wa Jumapili katika dimba la Stamford Bridge ili kuweza kupunguza pengo la pointi dhidi ya viongozi wa ligi Manchester City.

Utakuwa mchezo mwingine utakaowakutanisha Jose Mourinho na klabu yake ya zamani. Mourinho alishinda makombe mawili mfululizo ya EPL baada ya kuwasili Darajani mwaka 2004 kabla hajafukuzwa katika mwezi wa kwanza wa msimu wa 2007-08, kabla ya kurudishwa tena mwaka 2013 na akabaki hapo kwa miaka 2 na nusu.

Mourinho, ambaye alijiunga na United katika kipindi cha kiangazi cha mwaka 2016, ameshinda mechi 5 kati ya 9 dhidi ya vilabu alivyowahi kuvifundisha katika maisha yake ya ukocha, amefungwa mechi 3 na sare 1.

Ushindi wa 1-0 dhidi ya Benfica ugenini ulimaliza mfululizo wa kupoteza mechi za ugenini dhidi ya vilabu vyake vya zamani.

Chelsea wanaingia katika mchezo wa Jumamosi wakiwa wana rekodi ya kupoteza mechi 1 tu kati ya 15 walizocheza vs United katika uwanja wa Stamford Bridge. Wameshinda 9 na kutoa sare 5. Msimu uliopita walimtandika Mourinho 4-0 darajani.

Taarifa za Mchezo

Head-to-head

▪ Chelsea wamepoteza mchezo 1 kati ya 15 iliyopita dhidi ya United katika uwanja wao wa nyumbani.

▪ Ushindi wa United wa 2-0 vs Chelsea ulimaliza ubabe wa Chelsea kucheza mechi 12 za ligi bila kupoteza vs United.

▪ United wamepoteza mechi nyingi za Premier League dhidi ya Chelsea ( mechi 17) na wameruhusu magoli 66 dhidi yao – idadi kubwa zaidi kuliko dhidi ya timu yoyote katika ligi hiyo.

Chelsea

▪Chelsea wameshafungwa mechi 2 za nyumbani msimu huu, idadi sawa na mechi walizopoteza darajani katika msimu wote wa Premier League.

▪ The Blues wamepata clean sheet 5 katika mechi 18 kwenye mashindano yote msimu huu.

▪ Antonio Conte ameshinda pointi 112 katika mechi 48 za Premier League alizoifundisha Chelsea, pointi 11 pungufu na zile alizopata Jose Mourinho alizopata wakati alipokuwa Chelsea.

.

▪ Chelsea wanaweza kuweka rekodi mbaya ya kupoteza mechi za nyumbani dhidi ya vilabu vya Manchester vyote ndani ya msimu 1978-79.

Manchester United

▪ United wana pointi 23 mpaka sasa, idadi kubwa zaidi baada ya mechi 10 za EPL tangu msimu ambao walishinda ubingwa kwa mara ya mwisho 2012-13.

▪ Ikiwa Manchester United wataepuka kipigo watakuwa timu ya kwanza kufikidha pointi 900 za Premier League katika historia ya ligi hiyo.

▪ Wamefunga magoli 10 kati ya 23 ya ligi ndani ya dakika 10 za mwisho za michezo.

▪ Jose Mourinho hajashinda mchezo hata mmoja wa ugenini vs vilabu vilivyoshika nafasi ya 6 za juu msimu uliopita- tangu alipokuwa kocha wa Man United.

▪ Hata hivyo Mourinho hajafungwa mechi 8 alizocheza vs mabingwa watetezi, ushindi mechi 3 na sare 5.

▪ Rekodi ya David de Gea kupata clean sheets tangu mwanzoni mwa msimu wa 2016/17 ndio rekodi bora kuliko golikipa yoyote katika ligi kubwa 5 barani ulaya.

Taarifa za kiafya za wachezaji

Chelsea – Bakayoko mwenye majeruhi ya groin, David Luiz (paja), Hazard (achilles), Kanté (hamstring), Morata (match fitnes) – wana hati hati ya kucheza.

Manchester United – Majeruhi Fellaini (goti), Pogba (hamstring, wote wanatarajia kurudi 18 Nov), Ibrahimovic (goti, Dec), Carrick (calf, unknown)

Rojo na Lingard wanaweza kuanzia benchi lakini wanakosa match fitness.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here