Home Ligi EPL Arsenal kuendelea kuwavimbia Manchester City leo?

Arsenal kuendelea kuwavimbia Manchester City leo?

2800
0
SHARE

Unawaona Arsenal kama vibonde na City kama watemi? Sikia hii, katika michezo 9 ambayo Manchester City amekutana na Arsenal, City ameshinda mara moja tu tena ilikuwa msimu uliopita pale Etihad .

Lakini ni wazi kwamba kwa sasa hakuna asiyeigopa Manchester City kwani katika michezo 10 tayari wana alama 28 ikimaanisha wamekosa alama 2 tu hadi sasa.

Kama Pep ataifunga Arsenal hii leo baasi atafikia rekodi ya Manchester City waliyoweka nwaka 1947 ya kushinda michezo 9 mfululizo katika msimu mmona wa ligiii.

Tayari Manchester City wamefunga jumla ya mabao 35 msimu huu rekodi ambayo inawatishia sana wapinzani wao huku Arsenal hadi sasa wakiwa wamefunga mabao 19 tu katika ligi kuu Uingereza.

Kama Arsenal watafungwa katika mchezo wa leo baasi watakuwa wamepoteza mchezo wao wa nne ugenini na hii itakuwa mara ya kwanza kupoteza michezo 4 kati ya 6 ugenini tangu mwaka 1981.

Lakini kocha Arsene Wenger ana jambo la kujigamba hii leo kwani ndio kocha pekee ambaye amewahi kumfunga Pep Gurdiola akiwa Barcelona, Bayern Munich na Manchester City.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here