Home Kimataifa Messi ashinda fidia ya mil. 200, kesi ya kutumia madawa ya kuongeza...

Messi ashinda fidia ya mil. 200, kesi ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu

6535
0
SHARE

Kampuni yenye jukumu la kusimamia haki za taswira ya Lionel Messi imetangaza kwamba mchezaji huyo ameshinda kesi ya udhalilishaji dhidi yake na kupata malipo ya fidia ya €70,000 – takribani millioni 200 za kitanzania.

Fedha hizo za fidia zimetokana na ushindi wa La Purga katika kesi dhidi ya gazeti la kihispaniola la “La Razon” ambalo lilichapisha habari kwamba mchezaji huyo anatumia dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku michezoni.

Messi aliwashtaki La Razón kutokana na makala iliyopewa jina la “Sonatina” iliyoandikaa na mwandishi Alfonso Ussía, ambaye kwenye makala hayo alimshambulia sana Messi, akipinga ushindi wake wa tuzo ya mchezaji bora wa 2014 FIFA World Cup, Ussía alisema Messi alicheza vibaya kwenye mashindano hayo ni kwasababu aliacha kutumia madawa anayotumiaga wakati wote, tuhuma ambazo ameshindwa kuzithibitisha mahakamani na jaji wa mahakama kuu akaamuru jarida hilo kumlipa Messi fidia hiyo, ambayo Messi aliitoa haraka iende kwa taasisi ya madaktari ya Doctors Without Borders ya nchini Ufaransa.

Doctors Without Borders, ambao wanafahamika kama Médecins Sans Frontières nchini kwao Ufaransa – ni taasisi ambayo tayari imeajiri watu 30,000 – wengi wao wakiwa madaktari na manesi na wanafanya kazi katika maeneo yenye vita na nchi zinazoendelea ambazo zimeathirika na magonjwa ya milipuko. Asilimia 90 taasisi hiyo inajiendesha kutokana na michango kutoka kwa binafsi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here