Home Kimataifa United, Barca, Juve, Bayern na PSG wanaitafuta 16 bora ya CL hii...

United, Barca, Juve, Bayern na PSG wanaitafuta 16 bora ya CL hii leo huku Chelsea akienda kujaribu kuondoa mkosi ya Kiitaliano

6515
0
SHARE

Katika michezo mitatu iliyopita As Roma na Chelsea hakuna mbabe kwani kila mtu ameshinda mara moja wakipata suluhu moja huku katika mchezo wa mwisho wakitoka suluhu ya bao tatu tatu.

As Roma wanaikaribisha Chelsea hii leo wakiwa na kumbukumbu ya kuwatembezea bao 3 kwa 1 mwaka 2008 katika uwanja wao wa Stadio Olimpico lakini habari njema kwa Chelsea ni kwamba leo Ngolo Kante anarejea huku katika kundi lao mchezo mwingine utakuwa kati ya Atletico Madrid dhidi ya Fc Quarabag 

Chelsea hawana imani kubwa na matokeo ya nchini Italia kwani siku za karibuni wana bahati mbaya na nchi hiyo huku wakiwa wameshapoteza michezo yao mitatu ya mwisho katika CL waliyocheza ugenini.

Wakati Chelsea wakienda Italia, Manchester United watakuwa eneo lao la kujidai la Old Traford uwanja ambao katika michezo 19 iliyopita United ya bara la Ulaya hawajapoteza mchezo hata mmoja wakisuluhu 4 na kushinda 15.


Manchester United wanakabiliana na Benfica huku ushindi wa leo dhidi ya Wareno hao utawafanya United kufudhu kwenda 16 bora ila hadi CSKA Moscow wapigwe au wasuluhu na Basel hii leo.


Benfica wanaonekana wanyonge sana wanapoenda kuikabili United kwani katika michezo 10 Benfica wamepata ushindi mara moja tu huku United wakifanikiwa kupata bao katika kila mchezo dhidi ya Benfica.


Matumaini ya Olympiakos kufudhu kwenda 16 bora yanaonekana yanaweza kukatika hii leo watakapokabiliana na Barcelona kwani wakikubali kupoteza na Juve akamfunga Sporting baasi habari ya Olympiakos itaishia hapo.


Matokeo ya ushindi kwa PSG dhidi ya Anderchelt yatawafanya nao wafudhu kwenda hatua ya 16 bora lakini nao watategemea matokeo ya Celtic ambao wakishindwa kupata ushindi dhidi ya Bayern Munich baasi PSG atafudhu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here