Home Ligi EPL Alvaro Morata anataka kuondoka Chelsea asubuhi yote hii?

Alvaro Morata anataka kuondoka Chelsea asubuhi yote hii?

10721
0
SHARE

Ndio kwanzaa hata nusu ya msimu wa ligi kuu ya Epl hatujafika, lakini tayari mchezaji ambaye alikuwa gumzo sana wakati wa usajili Alvaro Morata ameshaanza kuzungumza maneno yanayotia hofu.

Alvaro Morata akizungumza na jarida moja nchini Italia alikiri kuikumbuka sana Italia huku akisema hajioni akikaa nchini Uingereza kwa muda mrefu na hana uhakika kama jambo hilo litatokea.

Morata ameweka wazi kwamba bado anakumbuka maisha ya nchini Italia na kati ya mambo yalikuwa yakimpa msongo wa mawazo ni kuhama katika nchi yenye tamaduni na watu wazuri kama Italy.

Lakink baada ya kauli za mwanzo za Morata kuzua utata ameibuka tena na kusema anaipenda Chelsea na kama wangempa hata mkataba wa miaka 10 angesaini.

Kiasi cha £70m kilimng’oa Alvaro Morata toka Real Madrid na kujiunga na Chelsea huku katika michezo 13 aliyoitumikia Chelsea akifunga jumla ya mabao 7 katika klabu hiyo.

Kuhusu kasi yake ya ufungaji Morata amesema haimridhishi kwa sasa na anafahamu wazi kwamba kama asipofunga mabao baasi itawalazimu Chelsea kutafuta mshambuliaji mwingine anayefunga.

Wakati Alvaro Morata akizungumza hayo, kocha wa Chelsea Antonio Conte amesisitiza kwamba Morata ni mtu mzuri sana na mara nyingi alipokuwa akiongea naye ameonekana kijana anayependa Chelsea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here