Home Kitaifa Omog amewapinga wanaobeza safu ya ulinzi Simba

Omog amewapinga wanaobeza safu ya ulinzi Simba

6344
0
SHARE

Baada ya Simba kuruhusu goli lililotokana na umakini mdogo wa mabeki kwenye mchezo wa watani wa jadi, kocha mkuu wa Simba Joseph Omog amekanusha kwamba kikosi chake kina safu mbovu ya ulinzi.

Simba waliruhusu goli hilo liloanzia kwa Ajib ambaye hakukabwa kwa usahihi na Mwanjale akapata nafasi ya kutoa pasi kwa Mwashiuya ambaye hakuwa amekabwa akapiga pasi iliyomkuta Chirwa akiwa anaangaliwa na Juuko pamoja na Zimbwe Jr akafunga kwa urahisi.

“Sio kwamba safu yetu ya ulinzi ni mbovu, unapopoteza umakini wakati wowote unaweza kufungwa, lakini tuna mabeki wazuri. Wakati tunacheza dhidi ya Yanga tulipoteza umakini mara moja tukaruhusu goli rahisi”-Omog.

Omog pia amesema mchezo wa Simba na Yanga mara zote huwa mgumu kwa sababu unakutanisha timu mbili bora nchini.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here