Home Kitaifa Hatimaye Kagera Sugar imepata ushindi wa kwanza VPL

Hatimaye Kagera Sugar imepata ushindi wa kwanza VPL

2490
0
SHARE

Jumapili ya October 29, 2017 Kagera Sugar imepata ushindi wa kwanza tangu kuanza kwa msimu huu baada ya kuifunga Ndanda 2-1 kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

VPL 2017/18 imeanza tangu August 26, 2017 lakini Kagera Sugar walicheza mechi nane mfululuzo bila ushindi. Sare na kupoteza ndio yalikuwa matokeo yao katika mechi saba zilizopita.

Kama unakumbuka, msimu uliopita Kagera Sugar ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi nyuma ya Yanga na Simba huku wakiwa juu ya Azam. Mecky Maxime akachaguliwa kuwa kocha bora wa msimu huo baada ya kuisaidia timu yake kumaliza katika nafasi nzuri.

Matokeo mabovu ya msimu huu yalianza kuzua maswali mengi kwa timu hiyo yenye wachezaji mchanganyiko wa vijana na wazoefu wa ligi kuu Tanzania bara.

Matokeo ya Kagera Sugar tangu kuanza kwa msimu huu (2017/18)

 • Kagera Sugar 0-1 Mbao
 • Kagera Sugar 1-1 Ruvu Shooting
 • Azam 1-0 Kagera Suga
 • Singida Unied 1-0 Kagera Sugar
 • Majimaji 0-0 Kagera Sugar
 • Kagera Sugar 1-2 Yanga
 • Mwadui 1-1 Kagera Sugar
 • Kagera Sugar 2-1 Ndanda

Majimaji na Ruvu Shooting ndio timu pekee ambazo hazijashinda hadi sasa katika mechi za ligi kuu Tanzania bara.

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo October 29, 2017

 • Lipuli 2-1 Mbao
 • Mtibwa Sugar 0-0 Singida United
 • Njombe Mji 0-0 Stand United
 • Majimaji 1-1 Mwadui

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here